October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Diamond Platnumz kuachia EP Machi

Spread the love

STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amewatangazia mashabiki wake kwamba ataachia EP yake ya kwanza kabisa katika muziki. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Diamond ni msanii ambaye amepata umaarufu zaidi Barani Afrika kutokana na bidii katika kazi zake lakini ngoma zake nyingi kukubalika.

Vibao vyake vimekuwa vikipokea zaidi ya mamilioni huku familia yake ikizidi kuchanua kwa kupata umaarufu mkubwa nchini Tanznaia.

Safari ya muziki ya msanii huyo inafahamika na kutambulika na wengi, kwani alianza na mwanzo wa chini huku akiinuka siku baada ya siku.

Aidha, msanii huyo aliwauliza mashabiki wake kutoa majina ya EP yake.

“YES! March 4th 2022 My first EP in Music Life… Guess the tittle?Tareh 04, 03 2022 EP ya kwanza katika maisha ya Muziki wangu… Unazani Tuuitaje?,” aliandika Diamond.

error: Content is protected !!