KANISA la Maombi na Maombezi kwa Mataifa yote (RUTACH) limepiga marufuku waumini wake kuacha mara moja kukata mauno pindi wanapokuwa wakiimba kwaya au katika kipindi cha sifa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea)
Katazo hilo limetolewa leo tarehe 20 Februari, 2022 na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Living Mwambapa alipokuwa akihubiri katika ibada maalumu ya nguvu ya kulikomboa taifa na kuwahimalisha viongozi wa ngazi zote.
Mwambapa amesema kanisa siyo sehemu ya kufanya mambo yanayoshabihiana na yale ya kishetani badala yake pawe sehemu ya kutafuta Mungu aliye hai.
“Natangangaza kwa makanisa yote kuachana na tabia ya kufanya huduma ya uimbaji kwa kukata mauno au kuvaa nguo ambazo hazina staha.
“Hatuwezi kuruhusu mitindo ya kishetani kuingia makanisani, kuvaa nguo ambazo hazina staha au kukata mauno wanapokuwa kwenye huduma kanisani kwa kufanya hivyo ni kuibua hisia za kuwaondoa katika uwepo wa Kimungu,” amesema.
Amesema haiwezekani kufanya kanisa kama sehemu ya kitega uchumi kwa kufanya mambo ambayo yanayofanywa na watu wa mataifa.
” Kanisa ni sehemu takatifu ya kumlilia Mungu kwa kuishi katika matendo ya kumpendeza Mungu,hatuwezi kuruhusu mavazi ya ovyo au kukata mauno wakati wa uimbaji.
“Makanisani kuna watu nao wana mwili na Roho, hivyo siyo jambo zuri kuingizana kwenye majaribu kwa kukata mauno au kuvaa nguo ambazo hazina utukufu” ameeleza Askofu Mwambapa.
Leave a comment