Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko DC Songwe akana kumtwanga ngumi binti, Polisi waanza uchunguzi
Habari Mchanganyiko

DC Songwe akana kumtwanga ngumi binti, Polisi waanza uchunguzi

Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalenga
Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe, limeanza uchunguzi wa madai ya Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalenga, kumshambulia kwa kumpiga ngumi msichana Florencia Mjenda na kumsababishia jeraha kwenye jicho la kulia, kwa kosa la kukaa katika jukwaa lisilosahihi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 6 Desemba 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Alex Mukama, baada ya video fupi inayomuonyesha msichana huyo akilalamika kushambuliwa na Simalenga, kusambaa mitandaoni.

Kamanda Mukama, amesema uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika, taarifa itatolewa kwa umma.

“Na sie tumeliona hilo, tunalifanyia uchunguzi ukikamilika tutatoa taarifa kwenye vyombo. Lakini tuna taarifa ya tukio hilo tumeliona sidhani kama liko kama ilivyoelezwa,” amesema Kamanda Mukama.

Katika video hiyo fupi, Florencia alidai tukio hilo lilitokea wakati yeye na wenzake walipokwenda kushiriki michezo ambapo walikaa katika jukwaa ambalo si sahihi, ndipo Simalenga alipowaita ambapo yeye alikwenda kumsikiliza kisha akaanza kumpiga.

Florencia anadai kuwa, baada ya Simalenga kuanza kumpiga alimuomba msamaha akimueleza yeye ni mgeni hivyo hakujua kama jukwaa hilo halikuandaliwa kwa ajili yao.

Hata hivyo, Simalenga amekanusha madai hayo akisema hakuna mtu aliyepigwa bali alitoa maelekezo.

“Hakuna mtu aliyepigwa kwa namna ambavyo imeelezwa, mimi nilichofanya ni kutoa maelekezo. Nilimshika mkono na aliniomba msamaha,” amedai Simalenga.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!