Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Jaji Mkuu mstaafu awatunuku wahitimu 943 ARU
ElimuHabari

Jaji Mkuu mstaafu awatunuku wahitimu 943 ARU

Spread the love
WAKUFUNZI 54 wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), wamepata ufadhili wa kusoma Shahada za Uzamili kupitia mradi unaolenga kufanya tafiti kutatua changamoto za Mkoa wa Dar es Salaam. Amaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kupitia mradi huo Wakufunzi wengine 46 wanafadhiliwa kusomea Shahada za Uzamivu PhD  na kwamba kupitia mradi huo wameanzisha kituo cha umahiri cha mafunzo ya uendelevu wa miji.

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Kwenye mahafali hayo wahitimu 943 walitunukiwa Shahada, Shahada za Uzamili na Shahada za Uzamivu (PhD) na Mkuu wa chuo hicho, Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande.

Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Balozi Salome Sijaona akizungumza kwenye mahafali hay oleo jijini Dar e Salaam.

Miongoni mwao, wanafunzi 883 walitunukiwa Shahada za awali, 52 Shahada za Uzamili, sita Shahada za Uzamivu (PhD) na wawili Stashahada.

Aidha, Profesa Liwa alisema pia chuo kimeshiriki katika tafiti 114 zinazolenga kutoa suluhisho kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo mazingira, ardhi, makazi ya watu na ujenzi wa miundombinu.

Alisema ARU inaendelea na miradi mikubwa minne chini ya ufadhili wa serikali ya Ubelgiji mmoja ukilenga kufanya tafiti zitakazotatua changamoto zinazolikumba Jiji la Dar es Salaam.

Profesa Liwa alisema changamoto hizo kwa kiasi kikubwa zimechangiwa na uendelezaji holela wa Jiji la Dar es Salaam na kwamba mradi huo unatoa ufadhili kwa kusomesha wakufunzi wake.

Vile vile, (ARU), kimepokea shilingi bilioni 67.7 kupitia mradi wa upanuzi wa vyuo vikuu unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) ujulikanao kama Higher Education for Economic Transformation (HEET).

Msafara ukingia kwenye viwanja vya mahafali hayo ya 16 ambayo yamefanyika leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam

Profesa Liwa alisema mradi huo ni mkubwa kuwahi kutokea chuoni hapo kwani unabadilisha ukubwa wa miundombinu ya kufundishia na zana mbalimbali za kufundishia ikiwemo mitaala mipya ili kuendana na upanuzi wa chuo hicho.

Profesa Liwa alisema kwenye mradi huo chuo kimejikita kwenye utekelezaji wa maeneo nane ikiwemo ujenzi wa miundombinu mipya ya chuo na ujenzi wa kampasi mpya ya mkoani Mwanza.

Alisema wameshapata hati miliki ya eneo lenye ukubwa wa ekari 378, utayarishaji wa mpango kabambe wa eneo na michoro ya ujenzi na kwa michoro ya kampasi ya Dar es Salaam michoro ya majengo makubwa manne imekamilika na vibali vya ujenzi vimeshapatikana.

Sehemu ya wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi ARU wakiwa kwenye mahafali yaliyofanyika leo mchana maeneo ya chuo hicho Dar es Salaam

Alisema ujenzi wa kampasi ya Dar es Salaam umepangwa kuanza mwezi Machi mwakani baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi ya mshauri mwelekezi na mkandarasi.

“Kama kazi hizi zitatekelezwa kulingana na mpango kazi wetu, kazi hii inatarajiwa kukamilika mwaka 2024 kama inavyofahamika chuo chetu ndicho pekee kilichobobea kwenye masuala ya ujenzi hivyo wataalamu wetu wa ndani wametusaidia katika uandaaji wa nyaraka na michoro ya ujeni,” alisema Profesa Liwa

Alisema kwa mwaka wa masomo 2022/23 chuo kimefanikiwa kudahili wanafunzi 2,035 kwa Shahada za awali na jumla ya wanafunzi 86 kwa Shahada za Uzamili ambayo ni ongezeko la asilimia 1.3 kulinganisha na mwaka wa masomo uliopita.

Alisema ongezeko hilo siyo kubwa kulinganisha na malengo ya chuo ambalo ni kuongeza udahili wawanafunzi kutoka 6,657 wa sasa hadi kufikia wanafunzi 11,000 mwaka 2029.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

error: Content is protected !!