Monday , 4 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu
Afya

DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu

Spread the love

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za afya na maji kushirikiana ili kuainisha idadi ya visima vilivyopo ndani ya wilaya hiyo na kuvipima kubaini maji ya visima hivyo yana usalama kiasi gani kwa matumizi ya binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkuu huyo wa wilaya ametoa maagizo hayo leo Ijumaa  katika kikao kazi maalum cha kuweka mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu.

Amesema kila kaya inatakiwa kuzingatia suala la usafi wa mazingira, ikiwemo kunawa maji tiririka sanjari na kuwataka watumishi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kuweka nguvu kazi katika kutunza mazingira, hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

Amewataka maofisa afya kufanya ukaguzi katika maeneo ya kutolea huduma ya chakula, stendi za mabasi na maeneo mengine yanayohusisha mkusanyiko wa watu, ikiwemo maeneo ya mabucha ili kuhakikisha udhibiti unaimarishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

AfyaTangulizi

Kitita cha NHIF kuanza Ijumaa, kuwapa wanachama nafuu zaidi

Spread the love  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetangaza...

Afya

Dk. Biteko aagiza uboreshaji huduma za afya kwa wazee

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the loveWataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa...

error: Content is protected !!