Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Papa Francis: Starehe ya tendo la ndoa ni zawadi kutoka kwa Mungu
Habari Mchanganyiko

Papa Francis: Starehe ya tendo la ndoa ni zawadi kutoka kwa Mungu

Spread the love

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kwamba furaha ya tendo la ndoa ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo inapaswa kutendwa kwa na nidhamu na uvumilivu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Pia ameonya waumini wa kanisa Katoliki kuacha kujiingiza matumizi ya picha na video za ngono ‘ponografia’, ambayo alisema inawafanya binadamu kuridhika bila kuingia katika uhusiano na inaweza kusababisha uraibu.

Papa ametoa kauli hiyo juzi Jumatano katika mkutano wa kidini uliolenga kuonya jamii kuhusu maovu ya tamaa. Mkutano huo ulifanyika katika Muwanja wa Mtakatifu Petro jijini Vatican.

Hotuba hiyo ambayo ni sehemu ya mfululizo wa mahubiri kuhusu tabia mbaya na njema, ililenga kile Papa alichokiita “pepo wa tamaa”.
Papa alisema kwamba tamaa huharibu uhusiano kati ya watu.
“Je, ni mahusiano mangapi ambayo yalianza kwa njia bora na baadaye yamegeuka kuwa mahusiano yenye sumu?” Aliuliza.

Papa alitoa maoni hayo siku chache baada ya mkuu wake mpya wa mafundisho, Kadinali Victor Manuel Fernández, kulaumiwa kwa kitabu alichokiandika na kuchapishwa mwishoni mwa miaka ya 1990 kiitwacho Mystical Passion: Spirituality and Sensuality.

Kitabu hicho, ambacho chapa zake zimeisha, kilijadili kwa kina jinsia zote mbili na kutoa maelezo ya kina ya uzoefu wa kiume na wa kike wakati wa kilele.

Akizungumzia chapisho la mtandaoni la Kikatoliki la Crux, Kadinali Fernandez alisema aliandika kitabu hicho alipokuwa mdogo na hakika asingekiandika sasa.

Wachambuzi wa kihafidhina wamekiita kitabu hicho kuwa kinapotosha, huku mmoja akisema ilionyesha Kardinali Fernandez hafai kuwa gavana wa Dicastery for the Doctrine of the Faith.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!