Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Umeme wa jotoardhi kuzalishwa 2025
Habari Mchanganyiko

Umeme wa jotoardhi kuzalishwa 2025

Spread the love

SERIKALI imesema inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya umeme itokanayo na nishati jadidifu ya jotoardhi katika maeneo mbalimbali nchini kupitia Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Rasilimali ya Jotoardhi iliyofanyika  leo tarehe 18 Januari 2024.

Miradi ya kuzalisha umeme kutokana na Jotoardhi inayoendelea kutekelezwa nchini ni Ngozi 70MW na Kiejo – Mbaka 60MW iliyopo Mbeya, Sogwe 5MW, Luhoi 5MW mkoani Pwani na Natron 60MW uliopo Arusha.

“Kati ya miradi hiyo mitano, miradi minne ipo katika hatua ya uhakiki wa rasimali ya Jotoardhi na mradi mmoja wa Natron upo katika hatua ya utafiti wa kisayansi wa kina,” amesema Naibu Waziri Kapinga.

Amesisitiza kuwa suala la sheria ya uendelezaji miradi ya Jotoardhi litafanyiwa kazi na Serikali ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2025/2026  kuwe na uzalishaji wa Megawati 30 kutokana na umeme wa Jotoardhi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mathayo David amepongeza Serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme inayotokana na Jotoardhi.

Semina hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga na Watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya Uendelezaji ya  Jotoardhi Tanzania (TGDC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!