Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TEF yafariji waathirika mafuriko Kilosa
Habari Mchanganyiko

TEF yafariji waathirika mafuriko Kilosa

Spread the love

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) leo Alhamisi limekabidhi msaada wa kiutu kwa waathirika wa mafuriko wilayani Kilosa mkoani Morogoro yaliyotokea hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Msaada huo wa vyakula na nguo za watoto na wakubwa umewasilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Jukwaa hilo, Jane Mihanji, kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka.

Akikabidhi msaada huo, Mihanji amesema umetokana na kuguswa kwao na janga hilo lililoleta athari kubwa kwa wakazi wa Kilosa.

Amesema mbali na wao kufanya kazi ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha jamii, kiubinadamu wameguswa na majanga ya asili yaliyowakuta Watanzania wenzao, hivyo waliamua kuchangishana na kuwasilisha msaada huo kunakohusika.

Shaka, akipokea msaada huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, ameishukuru TEF kwa kujitoa kwao.

Shaka ameomba ushirikiano kati ya TEF na Serikali udumishwe, huku akiwahakikishia wahariri hao kuwa msaada huo utafika kwa walengwa kama ilivyokusudiwa.

Shaka amesema jamii wilayani Kilosa inatoa shukrani za dhati kwa wadau waliowafariji waathirika kwani kutoa ni moyo, si utajiri.

TEF iliwakilishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Anita Mendoza; Mjumbe Kamati ya Utendaji Jane Mihanji na Mjumbe Rashid Mtagaluka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!