Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Dawa mpya bora ya Ukimwi yaidhinishwa, matumaini yarejea
Kimataifa

Dawa mpya bora ya Ukimwi yaidhinishwa, matumaini yarejea

Spread the love

 

MAMLAKA inayoshughulika na uidhinishaji Dawa na Chakula nchini Marekani (FDA) imeidhinisha dawa inayoweza kutibu ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa watu wazima kwa kuitumia mara mbili kwa mwaka. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Wagonjwa wanapewa dawa hiyo mara mbili kwa mwaka kwa njia ya kudungwa sindani au kumeza tembe. Dawa hiyo inagharimu dola 42,250 za Marekani (sawa na Sh 99 milioni) kwa awamu hizo mbili.

Watumiaji pia wanahitajika kutoboka dola 39,000 (Sh91.1 milioni) kila mwaka kugharamia dozi za utunzaji.

Wakati huu, dawa sawa na hiyo inayojulikana kama Cabenuva (cabotegravir and rilpivirine) kutoka kampuni ya dawa ya Uingereza ya GSK, inagharimu dola 40,000 hadi dola 50,000 (Sh93.4 milioni hadi Sh117 milioni) kwa mwaka.

Mwaka 2021, dawa hiyo ambayo mgonjwa hupewa kwa kudungwa sindano, ilikuwa ya kwanza kuidhinishwa na FDA kama tiba ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya HIV.

Kulingana na wataalamu, dawa ya sasa inayojulikana kama Sunlenca (lenacapavir) inatumiwa kutibu watu ambao miili yao ni sugu kwa dawa mbalimbali.

“Uidhinishwaji huo unachangia uwepo wa aina mpya ya dawa ambayo inaweza kusaidia wagonjwa wa Ukimwi ambao wameshindwa kupata usaidizi wa dawa zingine. Kupatikana kwa dawa hii sasa kunaweza kusaidia watu hao kuwa buheri wa afya kwa kipindi kirefu,” alisema Dk. Debra Birnkrant, Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Ukimwi katika Kituo cha FDA cha Kufanyia Utafiti wa Dawa.

Sunlenca ndio dawa ya kwanza ya kudhibiti virusi vya HIV kuwahi kuidhinishwa na shirika la FDA.

Inafanya kazi kwa kulemaza ukuaji wa kirusi kinachojulikana kama HIV-1.

FDA iliidhinisha matumizi ya dawa hiyo kwa misingi ya majaribio yaliyohusisha wagonjwa 72 wenye virusi vya HIV.

Wagonjwa hao ni wale ambao walikuwa na kiwango cha juu cha virusi hivyo, hali iliyowafanya aina zingine za dawa kutofanya kazi katika miili yao.

Wakati wa majaribio hayo, dawa hiyo ya Sunlenca au placebo ilipewa wagonjwa katika kundi la kwanza huku nyingine kwa jina, ‘open-label Sunlenca’ ilipewa kundi la pili.

Ilibainika kuwa asilimia 87.5 ya wagonjwa waliopokea Sunlenca walishuhudia kupungua kwa viwango vya virusi ndani ya siku 14 za kwanza ikilinganishwa na asilimia 16.7 ya wagonjwa waliopewa placebo.

Baada ya wiki 26, asilimia 81 ya wagonjwa waliotumia Sunlenca kwa pamoja na dawa zingine za Ukimwi hawakupatikana na kiwango chochote cha virusi vya HIV baada ya kupimwa.

Sunlenca hutumiwa pamoja na dawa zingine za kudhibiti HIV. Dozi ya kwanza hutumiwa kwa njia ya vidonge na kudungwa.

Baadaye mgonjwa atadungwa dawa hiyo kila baada ya miezi sita. Wagonjwa waliotumia dawa hiyo huhisi kichefuchefu na maumivu sehemu ya mwili iliyodungwa lakini baada muda hali hiyo hupungua na mwili wa mgonjwa hurejesha kinga dhidi ya makali ya virusi.

Hata hivyo, bei ghali ya dawa hiyo inamaanisha kwamba huenda ikachukua muda hadi pale mashirika yatajitokeza kufadhili upatikanaji wake kwa ajili ya matumizi ya watu wengine walio katika mataifa yenye umaskini mkubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!