ZAIDI ya wananchi elfu tano wa Kijiji cha Msimba wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji safi na salama baada ya serikali kutumia shilingi milioni 400 kukamilisha kuufufua mradi wa maji uliotelekezwa na wajerumani miaka zaidi ya 60 iliyopita. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).
Akitoa taarifa ya mradi huo,mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira MORUWASA Mhandisi Tamimu Katakweba alisema awali wananchi hao walikuwa wakitumia hayo jana mbele ya Waziri wa maji Jumaa Aweso alipotembelea na kuzindua mradi huo.
Katakweba alisema wakazi hao walilazimika kutumia maji ya visima na mito kutokana na kukosa huduma ya uhakika ya maji safi na salama.
Alisema juhudi za kusogeza maji kwa wananchi ni safari ya kufikia malengo ya asilimia 85 ya upatikanaji wa maji Vijijini ikizidi kushika kasi na kutatua changamoto ya maji kwa wananchi.
Mkurugenzi wa MORUWASA alisema hiyo ni hatua nzuri ya mafanikio kama wataalamu kwa kuona sasa wananchi wanaaza kunufaika na miradi ya maji ukiwemo mradi huo utakaohudumia wakazi wa vijiji mbalimbali ikiwemo vya Mikumi na Msimba.
Naye Waziri wa maji Jumaa Aweso aliwaagiza wananchi wa vijiji hivyo kutunza vyanzo na miundombinu ya miradi ya maji uliotelekezwa hapa na serikali ya kikoloni miaka zaidi ya sitini iliyopita ambapo sasa serikali imeufufua kwa lengo la kuendeleza dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.
Nao wananchi wa kijiji cha Msimba waliishukuru Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha wanapata maji safi waliyoyakosa kwa miaka mingi
Leave a comment