April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Corona yatua Kenya

Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya Kenya

Spread the love

KENYA inakuwa nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuripotiwa kugundulika kwa mtu mwenye virusi vya Corona (COVID-19, mamlaka ya nchi hiyo imethibitisha. Inaripoti mitandano ya kimataifa … (endelea).

Leo tarehe 14 Machi 2020, Mutahi Kagwe  ambaye ni Waziri wa Afya nchini humo, amewaeleza wananchi wa taifa hilo kwamba, mgonjwa wa kwanza tayari ameripotiwa.

Amesema, Mkenya mmoja aliyetoka nchini Marekani kupitia London, Uingereza na kwasili nchini humo tarehe 5 Machi 2020, amekutwa na virusi hivyo.

”Tarahe 5 mwezi Machi aligunduliwa kuwa na virusi hivyo katika maabara ya serikali, lakini sasa viwango vyake vya joto vimeshuka na kuwa vya kawaida.

“Anakula vizuri lakini hawezi kutolewa hadi virusi hivyo vitakapokwisha mwilini,” amesema.

Waziri huyo amesema, kwamba kisa hicho ni cha kwanza kuripotiwa nchini Kenya tangu kuzuka kwa mlipuko huo mjini Wuhan, China.

Kagwe  amesema, kwamba mgonjwa huyo ambaye ni mwanamke, yuko katika hali njema. Pia amewataka Wakenya kuwa watulivu na kutokuwa na wasiwasi.

Amesema kwamba serikali ya Kenya kupitia wizara ya afya itaendelea kuimarisha mikakati ili kuhakikisha kwamba hakuna usambazaji wa virusi hivyo zaidi.

error: Content is protected !!