April 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema wamaliza kazi, Mbowe kuliona jua leo

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekamilisha mchakato wa kumtoa kifungoni mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, aliyekuwa anatumikia kifungo cha miezi mitano kwenye Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa na Benson Kigaila, Kaimu Katibu Mkuu Chadema, wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 13 Machi 2020 jijini Dar es Salaam.

Kigaila amesema, Chadema imeshalipa Sh. 70 milioni, faini aliyopigwa Mbowe dhidi ya hukumu iliyotokana na kesi ya uchochezi Na. 112/2018 iliyokua inamkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

“Mbowe tushamlipia tayari, kinachotakiwa baada ya hapa ni kumpokea. Mjipange tumpokee na tukatae kitendo ambacho polisi wanatufanyia kuzuia misafara yetu,” amesema Kigaila.

Ezekiel Wenje, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya kuchangisha fedha za kuwakomboa viongozi wakuu wa amesema wamefunga zoezi hilo.

Wenje amesema, zoezi hilo limefungwa baada ya kukusanywa Sh. 312 milioni kati ya Sh. 300 milioni, zilizokua zinahitajika.

“Kupitia Watanzania mbalimbali mama ntilie na bodaboda, tumefanikiwa kupata mil. 312. Nasema kwa ujasiri kazi tumeikamilisha.Namba zote kuanzia sasa tumezifunga rasmi hazitapokea michango,” amesema Wenje.

error: Content is protected !!