April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Corona inavyoitoa machozi dunia

Spread the love

DUNIA inatikisika, virusi vya ugonjwa wa Corona vimeendelea kusamba na kusababisha hofu kubwa sambamba na vifo. Anaandika Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Shughuli za uzalishaji zimepungua, michezo na burudani pamoja na mikusanyiko, sasa vimepigwa marufuku sehemu mbalimbali dunia, chanzo ni Corona (COVID-19).

Kama mdhaha vile, picha na video mbalimbali zilikuwa zikionesha raia wa taifa la China wakiwa wamevaa vitambaa puani (mask), pengine dunia haikuona uzito wa jambo hilo, kila taifa likaendelea na mipango yake lakini sasa, hali inatisha.

Jiji la Wuhan nchini China ndilo lililoanza kutikiswa, kisha virusi vya ugonjwa huo vikaanza kupiga mwendo kwenye majimbo mengine na hata nje ya mipaka ya taifa hilo.

Tayari nchi zaidi ya 100 duniani zinahaha kutafuta salama kutokana na virusi vya ugonjwa huo, ugongwa huo umewakumba viongozi wa serikali, watu maarufu na kusababisha vifo.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, China inongozwa kwa kuathirika na mlipuko huo, ambapo ina vifo 3,176 ikifuatiwa na Italia (1,016), Irani (429), Hispania (87), Korea Kusini (67), Ufaransa (61), Marekani (41), Japan (17) na Uingereza (10).

Kwa sasa madaktari tisa wa China wamewasili nchini Itali kwa ajili ya kutoa msaada, katika kukabiliana na janga hilo. Madkatri hao wanatarajia kusambaza tani 31 za dawa za kuangamiza virusi hivyo.

Nchi ya Italia ina watu 12,000 walioambukizwa virusi vya Corona, na vifo vya watu 1,016.

Sophie Gregoire Trudeau, Mke wa Waziri Mkuu Canada, Justin Trudeau amekutwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Vile vile, Peter Dutton, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Australia naye anahangaika kuokoa maisha yako baada ya kubainika kushambuliwa na virusi hivyo.

Mohammad Mirmohammadi (71), ambaye alikuwa mshauri wa kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei tayari amezika kutokana na maradhi hao.

Mke wa Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau aitwaye Sophie Gregoire Trudeau naye ametengwa na yupo chini ya uangalizi kutokana na kukutwa na virusi vya corona.

Mwigizaji na mtunzi kutoka Hollywood, Rita Wilson amekutwa na maambukizi ya virusi hivyo ambapo yeye na mumewe wametengwa.

Katika michezo, virusi hivyo vimeendelea kuwa tishio na hata kusababisha kubadilika kwa taratibu na kanuni za michezo pamoja na kuahirishwa kwa mechi.

Mechi kati ya Arsenal na Brighton iliyopangwa kufanyika leo tarehe 14 Machi 2020, imezuiwa kutokana na Mikel Arteta, kocha wa Arsena kukutwa na virusi vya ugonjwa huo.

Lakini pia Callum Hudson Odoi, mchezaji wa Chelsea naye ameingia kwenye orodha ya watu walioambukizwa virisi vya Corona na kuingiza hofu kwenye klabu hiyo.

Watu wa karibu wa Arteta na Odoi wamewekwa chini ya uangalizi maalumu wa wataalamu wa afya kwa muda wa siku 14, ili kujua kama wameambukizwa ama la.

Italia tayari imefunga makanisa yote kutokana na virusi vya ugonjwa huo kusambaa kwa kasi, serikali imepanga kufunga baa zote na kuzuia mikusanyika.

Austarilia tayari imetoa tangazo la kutoruhusu mkusanyiko wa watu kuanzia 500, ikiwa ni hatua za awali kuelekea taratibu zingine za kuikabili Corona.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), jana imeripoti mtu wa pili aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona huku Misri, Morocco zikiendelea kupambana kuzuia maambuzi mapya ya virusi hiyo.

error: Content is protected !!