May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Corona: Bila kutimiza masharti haya, hupandi mwendokasi

Spread the love

 

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), umetoa maelekezo kwa abiria wanaotumia usafiri huo jijini Dar es Salaam, wa namna bora ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kwa umma, iliyotolewa jana Jumatatu tarehe 22 Februari 2021, na Kitengo cha Mawasiliano cha Dart, imeeleza masharti sita ambayo abiria anapaswa kuyazingatia.

Miongoni mwa masharti hayo ni; kunawa mikono kwa kutumia maji safi tiririka na sababu vilivyowekwa katika vituo vya mabasi na kuvaa barakoa muda wote unaposafiri na mabasi ya Dart, hususan nyakati za asubuhi na jioni.

Pia, Dart imesema, barako inapaswa kuwa imeidhinishwa na wizara ya afya kupitia Bohari ya Madawa ya Taifa (MSD), ama za kitambaa za kujishonea mwenyewe.

error: Content is protected !!