May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Balozi wa Italia auawa DRC

Luca Attanasio

Spread the love

 

LUCA Attanasio, Balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ameuawa katika shambulio lililolenga magari ya Umoja wa Mataifa (UN). Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Luigi Di Maio, Waziri ya Mambo ya Nje ya Italia ameeleza, balozi wake ameuawa jana tarehe 22 Februari 2021, sambamba na mwanajeshi wa taifa hilo baada ya msafara kushambuliwa na waasi.

“Kwa masikitiko makubwa, wizara ya mashauri ya kigeni inathibitisha kifo cha balozi kilichotokea jana, mjini Goma,” taarifa ya wizara imesema.

Sambamba na vifo hivyo, dereva mmoja raia wa DRC naye aliuawa. shambulio hilo lilitokea karibu na Mji wa Kanyamahoro uliopo Mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa zaidi zinaeleza, lengo la waasi kufanya shambuli hilo, lililenga kuteka nyara, makundi hayo yamekuwa yakitumia Mbuga ya Wanyama ya Virunga kutekeleza uasi huo.

Mbuga hiyo inapakana na Rwanda na Uganda ambapo walinzi wake wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na hata kuuawa.

error: Content is protected !!