Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo ampa ujumbe mzito Dk. Nchimbi uteuzi CCM
Habari za SiasaTangulizi

Chongolo ampa ujumbe mzito Dk. Nchimbi uteuzi CCM

Spread the love

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amepongeza Balozi Dk. Emanuel Nchimbi kwa kuteuliwa kurithi nafasi yake na kusisitiza imani ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwake katibu mkuu mpya ni kubwa sana na kwamba wana CCM hawana mashaka naye. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Chongolo ametoa kauli hiyo leo saa chache baada ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi kwa dharura leo Jumatatu kuridhia jina la Dk. Nchimbi kuchukua nafasi ya Chongolo aliyejiuzulu Disemba mwaka jana.

Jina la Nchimbi lilipendekezwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni maandalizi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu sambamba ma uchaguzi mkuu mwaka kesho.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chongolo aliyedumu kwenye nafasi hiyo kuanzia tarehe 30 Aprili 2021 hadi tarehe 28 Novemba 2023 ameandika hivi kumpongeza Dk. Nchimbi.;

“Hongera sana Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi kwa kuaminiwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan na kupendekeza jina lako na NEC kuridhia wewe kupeperusha bendera ya CCM kwa dhamana ya Mtendaji Mkuu, Katibu Mkuu.

“Imani ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwako ni kubwa sana nasi wana CCM hatuna mashaka nawe. Hongera saaana na kila lakheri!. #Kazilendelee,” ameandika Chongolo.

Chongolo alilazimika kujiuzulu, kufuatia kukumbwa na kashfa mbili nzito za kimaadili.

 Kashfa zilizotajwa kumuondoa kigogo huyo, ni madai ya udanganyifu yanayohusishwa kujipatia fedha za malipo ya bima; na madai ya kuvuja kwa mawasiliano yake ya kimapenzi aliyokuwa akiyafanya na mwanadada mmoja anayedhaniwa kuwa alikuwa mwandani wake.

Chongolo aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa CCM, tarehe 30 Aprili 2021. Alichukua nafasi ya Dk. Bashiru Ally, aliyefanywa kuwa Katibu mkuu Kiongozi na utawala wa Rais John Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!