Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa China yajitosa kulinda amani Afrika
Kimataifa

China yajitosa kulinda amani Afrika

Meli ya kivita ya Kijeshi ya China
Spread the love

JESHI la China inajipanga kuweka kambi ya kijeshi nchini Djibouti huku lengo mojawapo likiwa ni kulinda amani kwa nchi za Afrika na Magharibi mwa Asia, anaandika Catherine Kayombo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari China, tayari meli za kijeshi zimeondoka bandari ya Zhanjiang katika mkoa wa kusini wa Guangdong jana bila kutaja idadi ya wanajeshi au meli zilizopelekwa nchini humo kwa ajili ya kambi hiyo.

Kambi hiyo ambayo ni ya kwanza ya kigeni nchini Djibouti, itatumiwa kwa matumizi kadhaa ikiwemo kulinda amani barani Afrika na Magharibi mwa Asia, huduma za uokoaji, mazoezi ya kijeshi na kuimarisha ushikiano wa kijeshi baina ya nchi hizo mbili.

China imewekeza katika nchi za kiafrika na pia imeboresha kwa haraka jeshi lake miaka ya hivi karibuni. Kituo hicho cha Djibouti kimebuniwa kufuatiwa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili na kinaonekana kama moja ya hatua ya China kuwa na mamlaka ya kijeshi nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!