Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Rc Mongella achukua hatua kiwandani
Habari Mchanganyiko

Rc Mongella achukua hatua kiwandani

John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Spread the love

SERIKALI mkoani Mwanza, imekipa siku 10 kiwanda cha ngozi cha Mwanza Tanneries kilichopo Wilaya ya Ilemela jijini hapa, kuhakikisha kinaondoa vyuma chakavu mara moja ili kupisha uwekezaji mpya unaotarajiwa kuanzia muda wowote, anaandika Moses Mseti.

Kauli hiyo imetolewa na John Mongella, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea viwanda vilivyopo jijini hapa ili kujionea namna uzalishaji unavyofanyika na kukagua ujenzi wa babarabara ya njia nne unaoanzia mjini kati kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza.

Mongella amesema kuwa wamiliki wa kiwanda hicho wanapaswa kuondoa vyuma hivyo mara moja ili kupisha watu wengine wanaoweza kuwekeza ili waweze kukiendeleza kuliko eneo hilo kuendelea kutumika kutunza vyuma chakavu.

Amesema kuwa wamelazimika kuchukua hatua hiyo, baada ya kiwanda hicho cha ngozi kushindwa kuendelea na uzalishaji na kwamba kama hawataondoa vyuma hivyo ndani ya muda huo Serikali itachukua hatua nyingine itakazoona zinafaa.

Amesema kuwa miaka 50 iliopita mwasisi na Rais wa kwanza wa taifa hili, mwalimu Julius Nyerere na wenzake, walifanya kazi kubwa ya kuwekeza katika viwanda licha ya elimu yao kuwa ya wastani lakini wasomi na wenye elimu kubwa wameshindwa kufanya kazi kulingana na elimu zao.

“Mwalimu na wenzake uelewa wao ulikuwa mdogo, sasa hivi watu wana upeo ni mkubwa na ndio najiuliza wale waliwezaje kufanya mambo makubwa kama haya lakini leo watu wenye elimu na upeo hawafanyi jambo lililotukuka,” amesema Mongella.

Hata hivyo, Mongella amesema kwamba lengo la Serikali kutaka kuona ndani ya miezi sita kuanzia juzi kazi za uzalishaji katika kiwanda hicho iwe imeanza mara moja huku akidai kwamba hatajali mmiliki wa kiwanda hicho ana nafasi gani serikalini.

Chacha Mathew, Msimamizi wa Kiwanda hicho, amekiri kiwanda hicho kusitisha uzalishaji huku akidai wamepokea maelekezo hayo na kwamba atayafikisha kwa wamiliki wa kiwanda hicho ili kuangalia namna watafanya kuondoa vyuma chakavu.

Miongoni mwa wamiliki wa kiwanda cha Mwanza Tanneries, wanaotajwa kuwa ni aliyekuwa Mbunge wa Nzega mkoani Tabora, Rostam Aziz, licha ya msimamizi huyo kukataa kama ndiye mmiliki wa kiwanda hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!