Monday , 5 June 2023
Home Kitengo Michezo Rooney afunika Dar, Mwakyembe afurahia
Michezo

Rooney afunika Dar, Mwakyembe afurahia

Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akisalimiana na Wayne Rooney alipokuwa akiwasiri na timu yake ya Everton
Spread the love

IKIWA imebaki siku moja tu kufikia Julai 13, siku ya mechi ya Everton ya Uingereza na mabingwa wa Sportspesa, Gor Mahia itachezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, shauku ya Watanzania kumuona Wayne Rooney uwanjani inazidi kupamba moto, anaandika Jovina Patrick.

Everton imewasili nchini asubuhi kutoka Uingereza na washabiki wengi kumiminika katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuangalia kama ni kweli Rooney ameandamana na timu hiyo inayokuja kwa ajili ya mechi hiyo maalum.

Everton, klabu ya jijini London, inayoshiriki Ligi Kuu ya England na ikiwa ni timu maarufu barani Ulaya, imedhaminiwa na Sportspesa. Gor Mahia ilibeba ubingwa katika michuano iliyoshindaniwa na timu za Tanzania na Kenya.

Rooney, mshambuliaji wa kimataifa wa England, amewasili nchini na timu ya Everton, siku chache baada ya kuingia mkataba wa kuichezea katika Ligi Kuu, akitokea klabu ya Manchester United pia ya Uingereza ambako anajulikana alivyokuwa na mchango mkubwa katika mafanikio yake. Rooney amekuwa kipenzi cha wengi kutokana na uwezo mkubwa wa kufunga magoli matatu katika mechi moja – hat-trick.

Amechochea mvuto miongoni mwa washabiki wa soka nchini kwa kuwa ndiyo mara yake ya kwanza kuzuru Tanzania, nchi ambayo watu wake wanasifika kuipenda mno Ligi Kuu ya England kuliko ligi nyingine za barani Ulaya.

Rekodi ya kukumbukwa zaidi kuhusu ufundi wa Rooney katika ufungaji, ni tukio la Septemba 28, 2004 alipofunga magoli matatu siku Manchester United ilipopambana na Fenerbahce ya Uturuki kwenye uwanja wa Old Trafford, London.

Gor Mahia iliwasili nchini jana mchana ikitokea jijini Nairobi, tayari kwa pambano dhidi ya Everton ambalo linatarajiwa kuzikutanisha timu zisizofahamiana na kwa kweli zisizolingana kiwango.

“Ni mechi ya kihistoria ambayo kila mchezaji anatamani kucheza. Tunaisubiri kwa hamu kubwa Everton ili pia nasi tujenge historia yetu kimchezo,” anasema Harun Shakava, anayechezea kwenye ngome ya Gor Mahia.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa ujio wa timu hiyo utaibeba Tanzania, kuitangaza kimataifa kwa kuwa vyombo mbalimbali vya habari vitakuwa vikiiangaza Tanzania.

“Siku zote watakazokuwa nchini, wataifanya Tanzania itangazike, isikike kwani tayari hata SuperSport wamefunga mitambo yao hapa,” amesema Dk Mwakyembe akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, mashabiki walifika kuwaona kikiwemo kikundi cha Wacongoman waliokuja kumlaki mchezaji wao anayechezea timu hiyo, Yannick Bolasie.

Msafara wa Everton ambao ni mara ya kwanza kufika nchini, ulikuwa na msafara wa watu 80.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Yanga waitwa Ikulu kesho Jumatatu

Spread the love RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kesho Jumatatu, tarehe...

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

error: Content is protected !!