February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

China kutoa msaada wa Bil 60

Spread the love

RAIS wa China, Xi Jinping amesema serikali yake itatoa dola za kimarekani 60 bilioni katika mpango wake wa miaka mitatu wa ushirikiano na Afrika katika shughuli za maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Jinping ametoa ahadi hiyo leo Septemba 03 ,2018 wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaofanyika jijini Beijing nchini China.

Fedha hizo zinatarajiwa kusaidia bara la Afrika katika shughuli za ujenzi wa miundombinu, ushirikiano katika sekta ya biashara na huduma za afya.

Vile vile, Rais Jinping ameahidi kwamba nchi yake itatoa ushirikiano katika kuimarisha amani ya kudumu Afrika, hatua ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi za Afrika.

Kadhalika, Rais Jinping amesema China itatoa nafasi za mafunzo ya kilimo bora na mafunzo ya ufundi kwa watalaam kutoka nchi za Afrika ili kuchangia katika maendeleo ya uchumi.

error: Content is protected !!