March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF wawatia kitanzi waamuzi wanne

Spread the love

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania TFF, kupitia kamati yake ya uendeshaji wa ligi (Kamati ya Masaa 72) iliyokaa jumamosi imewatia hatiani waamuzi wanne wanao chezesha ligi kuu kwa kushindwa kutafsili sheria 17 za mchezo wa soka katika baadhi ya mechi walizocheza. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Waamuzi waliokutwa na rungu hilo ni Jimmy Fanuel, Jamada Ahmada, Athumani Lazi na Nicholas Makaranga.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kamati hiyo ilikaa na kupitia mikanda ya video ya baadhi ya michezo iliyokuwa na maamuzi yenye upungufu kutoka kwa waamuzi.

“Kamati ilipitia taarifa za michezo mbali mbali na kuangalia matukio yaliyojitokeza na ilifanya maamuzi kulingana na kanuni mbalimbali za mashindano za ligi husika,” amesema Wambura.

Hata hivyo katika hatua nyingine kamati hiyo ya Saa 72, imevipiga faini ya Sh. 500,000, klabu za Coastal Union, Mbao FC na Prisons kila mmoja kwa kushindwa kuwadhibiti washabiki wake.

error: Content is protected !!