MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Donald Ngoma bado ataendelea kuwa nje ya uwanja baada ya kuendelea kutibu jeraha lake la goti lililomsumbua kwa muda mrefu licha ya kwenda nchini Afrika Kusini kwa matibabu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Msemaji wa klabu hiyo, Jaffari Maganga amesema kuwa kwa sasa hawawezi kumtumia mshambuliaji huyo bila kupata kibari kutoka kwa daktari wa timu hiyo ambaye anafahamu lini Ngoma anatakiwa kurudi uwanjani kutokana na ratiba aliyompangia.
“Mshambuliaji huyo anasaubiri tarehe yake ili aweze kurudi uwanjani lakini mpaka sasa wanafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa hiyo hivi karibuni watawapokea na kujiunga na wenzao,” amesema Jaffar.
Ngoma ambaye alisajiliwa akitokea Yanga mwishoni mwa msimu wa 2017/18 lakini mpaka sasa ajafanikiwa kucheza mchezo wowote akiwa na timu hiyo licha ya viongozi wake kusema itamchukua wiki tatu tu kupona jeraha lake hilo la goti lakini mpaka sasa bado hali tete.
Katika hatua nyingine klabu ya hiyo inatarajia kucheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Arusha United inayoshiriki ligi daraja la kwanza kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji wao ambao hawakuweza kucheza katika michezo miwili iliyopita ya ligi kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Leave a comment