Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda
Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Maandamano Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa kanda kwa kufungua dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea nafasi hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Ijumaa na Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Benson Kigaila, zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi hizo katika kanda nne, Victoria, Serengeti, Magharibi na Nyasa, litafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 22 Aprili mwaka huu.

Taarifa ya Kigaila imesema kuwa, uchaguzi wa viongozi wa kanda hizo utafanyika Mei 2024.

“Fomu za kuomba kugombea nafasi za uongozi ngazi ya Kanda husika zinapatikana Ofisi za Kanda, kwa Makatibu wa Mikoa na katika tovuti ya Chama kuanzia tarehe 12 Aprili 2024. Mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 22 Aprili 2024 saa 10:00 jioni katika Ofisi za Kanda husika ,” imesema taarifa ya Kigaila.

Nafasi zinazogombaniwa katika uchaguzi huo wa kanda ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti, mweka hazina ngazi ya chama, pamoja na viongozi wa mabaraza ya Chadema ngazi ya kanda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!