Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Cecilia ateuliwa kugombea urais Tanzania
Habari za Siasa

Cecilia ateuliwa kugombea urais Tanzania

Cecilia Augustino Mwanga wa Demokrasia Makini
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemteua Cecilia Augustino Mwanga wa chama cha Demokrasia Makini kuwa mgombea urais wa Tanzania na Tabu Mussa Juma mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Cecilia ameteuliwa leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage ofisi za tume hiyo zilizopo Dodoma.

Cecilia amekuwa mgombea wa tano kuteuliwa kati ya 17 waliochukua fomu za uteuzi NEC.

Wengine waliokwisha rejesha fomu na kuteuliwa ni; John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Leopard Mahona wa NRA, John Shibuda wa chama cha Ada Tadea na Mutamwega Mgaiwa wa  SAU

Cecilia ni mwanamke wa kwanza kuteuliwa kugombea mwaka huu kati ya wawili waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo ya juu.

Mwingine aliyechukua fomu ni; Qeen Cuthbert Sendiga wa chama cha ADC.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa taarifa na habari mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!