Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yafuta chaguzi tano za UVCCM, tatu za UWT zasimamishwa
Habari za SiasaTangulizi

CCM yafuta chaguzi tano za UVCCM, tatu za UWT zasimamishwa

Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimefuta chaguzi tano za umoja wa vijana (UVCCM), pamoja na kusimamisha chaguzi tatu za Jumuiya ya Wanawake ya chama hicho (UWT), kutokana na sababu za ukiukwaji wa maadili ikiwemo rushwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 27 Septemba 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, akitangaza maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho, jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shaka, idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa kuwa chama hicho kinaendelea kupokea malalamiko kuhusu chaguzi hizo, huku mengine yaliyopokelewa yakiendelea kufanyiwa kazi.

Hata hivyo, hakutaja maeneo ambayo chaguzi hizo zimefutwa na au kusimamishwa.

“Hadi sasa hatuna idadi kamili ya chaguzi zilizofutwa bado mapema sababu tunaendelea kupokea malalamiko na bado tunayafanyia kazi. Mfano mpaka kufikia juzi kwa upande wa vijana chaguzi zaidi ya tano zimefutwa. Kwa upande wa wanawake kuna chaguzi zaidi ya tatu zimesimamishwa,” amesema Shaka.

Aidha, Shaka amesema chaguzi zilizofanyika kupata viongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, hakukuwa na malalamiko mengi.

“Uchaguzi wa vijana na wanawake tunaendelea kufanyia kazi na tunaendelea kufuatilia. Hata hayo matukio yaliyoripotiwa yamechukuliwa hatua kwa wakati. Maeneo yamekuwa na vitendo kinyume na maadili na upangaji safu,” amesema Shaka.

Shaka amesema “Mambo yote haya chama kimeangalia kwa karibu na nataka kuwahakikishia jicho la chama linaangalia kila hatua. Msisitizo wangu kwa upande wa chaguzi zilizoko mbele yetu tunafuatilia sana suala la rushwa.”

Akitangaza maamuzi ya halmashauri hiyo, Shaka amesema imefanya uteuzi wa mwisho wa wagombea katika chaguzi za viongozi wa CCM ngazi ya wilaya, zitakazofanyika tarehe 1 hadi 2 Septemba 2022.

Wakati huo huo, Shaka amesema NEC imeongeza muda wa zoezi la wagombea wa nafazi zake ngazi ya taifa, kuchukua na kurudisha fomu, kuanzia tarehe 1 hadi 5 Oktoba mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!