Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kampeni ya China dhidi ya Uyghurs ilivyoenea hadi Pakistan
Kimataifa

Kampeni ya China dhidi ya Uyghurs ilivyoenea hadi Pakistan

Spread the love

KAMPENI ya China dhidi ya Wauyghur imesambaa katika mipaka yake, na kuwakumba mamia ya Wapakistani ambao wanailalamikia China kwenye masuala ya imani zao katika eneo la Xinjiang ambalo lina takriban Wayghurs milioni 10. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Alice Su, Shashank Bengali, na Shah Meer Baloch, ni Watoto wa Sakandar Hayat mfanyabiashara walinukuliwa na Gazeti la Los Angeles Times, juu ya maswahibu yaliyoikumba familia yao wakiwa Uyghurs.

Hayat na mwanawe Arafat waliondoka kaskazini-magharibi mwa Uchina na kuvuka mpaka na kuingia Pakistan ambapo ni nyumbani kwao Hayat ili kuwa karibu na familia yake.

Hayat na Arafat wakiwa Pakistan walipokea simu iliyotoka kwenye makazi yake ya awali huko mkoani Xinjiang (China) kuwa mkewe aliwekwa kizuizini ambapo wawili hapo waliamua kukimbili kwenye mpaka wa China Pakistan na kujikuta wakiwa kwenye mikono ya Polisi wa China.

Hayati aliwaomba Polisi hao wasimtenganishe na familia yake “Msitutenganishe,”Polisi walimjibu kuwa watamrejesha mwanawe baada ya wiki moja lakini walipoteana kwa muda wa miaka miwili kutoka mwaka 2017 mpaka mwaka 2019 walilipoti Alice, Bengali, na Baloch.

Kitendo hicho kimedaiwa kuwa sehemu ya serikali ya China kulalamikiwa kuwapa wakati mgumu watu wa imani tofauti.

Gazeti la Los Angeles Times liliripoti kuwa Pakistan inaingia lawamani kutokemea matendo hayo yanayoendelea kwa raia wake kwa madai kuwa imekaa kimya ili kulinda ufadhili wake wanaopewa na Uchina

Gazeti hilo limeripoti kuwa raia hao wapo kwenye wakati mgumu kwa kuwa wanakosa msaada kwa serikali za pande zote mbili ili ya China na ile ya Pakistani.

“Ni vigumu sana kuacha moyo wako, watoto wako, kuishi mahali pabaya zaidi kuliko jela,” Hayat alisema.

Alice, Bengali, na Baloch  waliliripoti kuwa Hayat Aliwasihi maafisa wa China na Pakistani wapate taarifa kuhusu familia yake bila majibu hadi mwaka wa 2019 akiwa kizuizini.

Wale ambao wamekuwa ndani ya kambi wanasimulia hadithi tofauti. Mohammed, Muyghur kutoka kusini mwa Xinjiang ambaye amekuwa akifanya biashara kati ya China na Pakistan tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000, aliiambia Los Angeles Times kwamba alikuwa amezuiliwa kwa miezi saba.

Alikamatwa alipovuka mpaka mnamo Juni 2018, alisema, kisha akawekwa kwenye kambi huku mikono yake ikifungwa katika chumba chenye watu 35.

Anaeleza kuwa watu hao walikuwa kizuizini Uyghur walikuwa wakielezwa sera za kikomonisti na kukemewa walipokwenda kinyume na sera hiyo.

Anasema Pakistan licha ya kuwa taifa la Kiislamu haiwezi kupinga malalamiko raia wake na wale wa Uyghur kwa kuwa ni wanafaika wakubwa wa mradi wa miundombinu wa Belt na Road wa maili 2000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!