October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CCM wawarudisha Waitara, Kalanga

Mwita Waitara, Naibu wa Waziri wa TAMISEMI

Spread the love

KAMATI Kuu Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM imeteuwa wagombea watatu watakaokiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mdogo wa ubunge. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kamati hiyo iliyoketi leo tarehe 14 Agosti, 2018 jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dk. John Magufuli, imemteuwa Julius Kalanga aliyekuwa Mbunge wa Monduli kupitia Chadema, kugombea tena kwenye jimbo hilo.

Pia, imemteua Mwita Waitara aliyekuwa Mbunge wa Ukonga kupitia Chadema, kugombea tena kwenye jimbo hilo kupitia CCM. Vilevile, imemteua Timotheo Mzava kugombea katika jimbo la Korogwe Vijijini.

Waitara na Kalanga hivi karibuni walijivua uanachama wa Chadema pamoja na ubunge na kuhamia CCM, chama hicho kimewapitisha tena kugombea kwenye majimbo yao.

error: Content is protected !!