Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mwakyembe awaagiza TCRA kutoa ufafanuzi sakata la ving’amuzi
Habari Mchanganyiko

Dk. Mwakyembe awaagiza TCRA kutoa ufafanuzi sakata la ving’amuzi

Spread the love

DK.Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo,  amesema kuwa uamuzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzitaka kampuni zinazomiliki Zuku, DSTV na Azam TV kuondoa chaneli za umma katika mfumo wa kulipia umezingatia sheria. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Mwakyembe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Wizar ya Habari Maelezo kuhusu malalamiko yaliyoibuka hivi karibuni baada ya ving’amuzi hivyo kuondoa kabisa chaneli hizo ambazo ni pamoja na Star TV, Clouds TV, ITV, Channel 10 na EATV.

Amesema kuwa Serikali inataka Katiba ifuatwe kwa sababu kila Mtanzania ana haki ya kupata habari na hata katika kipengere cha 14 cha Katiba hakijataka wengine walipishwe ili kupata habari hivyo kilichozuiwa ni kutowalipisha watanzania chaneli ambazo ni za umma na Serikali haijaagiza kufungia chaneli ili watu wasipate habari.

“Chaneli zingine zinaendelea kama kawaida ispokuwa kuna zile program ambazo ni za (Free To Air) FTA zinazolenga mtanzania na kama wameamua kufunga ni utashi wao,” amesema.

Hata hivyo ameiagiza Mamlaka husika ambayo ni TCRA kutoa mwongozo wa nini kifanyike kwa ambao waliamua kuchukua leseni ya kutoa matangazo kwa kulipia.

Hata hivyo amesema kuwa kama kuna anayeona kuwa sheria yetu inaonekana ina mapungufu utaratibu upo wa kubadilisha sheria.

“Kama katika utekelezaji wa sheria hii na kama katika leseni yako kuna utata milango ipo wazi, weka juu ya meza sio lazima iwe TCRA unaweza ukaanzia Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kama kuna hoja ya msingi tupo tayari kusikiliza sisi hatujawahi kufunga vioo,” amesema.

Pamoja na hayo Mwakyembe amesema ni kiasi kikubwa cha fedha Kampuni hizo zimeweza kutengeneza kwa njia ambayo sio halali hivyo inaangalia namna ya kuchukua hatua kwa vyombo hivyo vilivyo kiuka sheria kwa kulipisha watanzania Chaneli za umma zinazotakiwa kuonekana bila kulipia.

Kwa mujibu wa Mwakyembe kwa wenye leseni za kuendesha matangazo kwa kulipia wanalipa Dola Mil. 1 huku wanaorusha matangazo bure yaani FTA wakilipa dola laki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

error: Content is protected !!