Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM wapanga kumuongezea muda Rais Mwinyi kukaa madarakani
Habari za SiasaTangulizi

CCM wapanga kumuongezea muda Rais Mwinyi kukaa madarakani

Spread the love

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinakusudia kupeleka hoja ya mabadiliko ya 13 ya Katiba ya Zanzibar ili kuwezesha kuongezewa muda wa muhula wa uongozi Dk. Hussein Ali Mwinyi ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

“Tunaanza rasmi kuipeleka hoja hii mbele ya Sekretarieti ya CCM Zanzibar tarehe 10 Januari, 2014 ili utaratibu uanze. Wala hatukushauri tumeamua sisi kwa sababu ilani ya CCM ya miaka mitano imeshaitekelza kwa miaka mitatu tu ya uongozi wako,” anasema Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar katika maelezo yake leo tarehe 6 Januari, 2024 mbele ya Rais Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la kisasa Mwanakwerekwe, Zanzibar.

Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar

Kwa mujibu wa maelezo ya awali ya viongozi wa CCM waliohudhuria hafla hiyo, inakusudiwa kuwa badala ya muhula wa uongozi wake kutimia 2025, Dk. Mwinyi amalize muhula wa kwanza mwaka 2027, miwili zaidi ya mitano inayoelekezwa na Katiba.

Rais Mwinyi aliingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, na Katiba inamruhusu kumaliza muhula mmoja mwaka 2025 na kama atagombea tena na kuchaguliwa, akamilishe mitano ya pili mwaka 2030 ambako atastaafu uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!