Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Oryx Gas Tanzania yagawa mitungi 700 Iramba – Singida
Habari Mchanganyiko

Oryx Gas Tanzania yagawa mitungi 700 Iramba – Singida

Spread the love

KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha, Dk.Mwigulu Nchemba wamegawa mitungi ya gesi ya gesi ya Oryx 700 pamoja na majiko yake kwa wananchi na wajasiriamali wakiwemo Baba na Mama Lishe. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza leo Jumapili katika hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Seleman Mwenda, Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas Tanzania, Benoit Araman ameendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Pia amewaomba Watanzania kuyatazama matumizi ya gesi ya kupikia nyumbani kuwa huduma muhimu na mwafaka katika kulinda afya ya jamii.

“Oryx Gas tunaamini ukipika kwa gesi  ya Oryx utakuwa unalinda mazingira kwa kuacha kukata kuni na mkaa lakini utakuwa unalinda afya ya wanawake kwa kuwaepusha kuvuta moshi na mvuke unaoathiri mapafu na afya yao unaotokana na kuni na mkaa.


“Wanawake wanatumia muda mchache kupika kwa gesi na hivyo wanapata nafasi kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuepuka kugombana na wenza wao kwa kuchelewesha chakula” amesema.

Pia amesema kupika kwa kutumia gesi ya Oryx, watoto wanapata muda mwingi wa kusomea na sio kwenda kutafuta kuni huku akisisitiza kutumia mtungi wa gesi ya Oryx pia kunamaanisha kulinda na kuboresha maisha ya wanawake kwa kuwazuia kwenda kukusanya kuni msituni.

“Kwa miaka mingi Oryx Gas imekuwa kampuni kiongozi katika kukuza matumizi ya gesi nchini. Kuanzia Julai mwaka 2021 tumekuwa mstari wa mbele kutekeleza maelekezo ya Serikali tulioyapokea kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi watumie nishati safi ya kupikia,” amesema.

Amesisitiza kupitia mipango hiyo, Oryx Gas inataka kutokomeza matumizi ya nishati chafu ya kuni na mkaa  ambayo si tu mbaya kwa afya bali pia ni hatari kwa mazingira.

Pia, alimshukuru Dk. Nchemba kuwa balozi mzuri wa kuleta maendeleo kwa wanawake na jamii kwa ujumla kwa kuiunga mkono Oryx Gas Tanzania katika mpango wa matumizi ya nishati safi mkoani  Singida.

“Tunafurahi kumkabidhi mitungi ya gesi 700 kwa wakazi wa Iramba yenye thamani ya Sh. milioni 50,”amesema Benoite.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iramba mkoani Singida, Seleman Mwenda aliyemwakilishia Dk. Mwigulu amesema jitihada za kuhamasisha nishati safi ya kupikia kwa kugawa mitungi ya gesi ya Oryx ni sehemu za  kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhimiza wananchi kutumia nishati safi ya kupikia.

“Kupika kwa gesi kunasaidia kutunza mazingira pamoja na afya hasa kwa baba na mama lishe ambao wanajihusisha  na shughuli za upishi kwani tumegundua misitu mingi inateketea kwa sababu ya matumizi ya kupikia,”amesema.

Pia amesema athari nyingi ambazo wanazipata baba na mama lishe zinatokana na mkaa pamoja na kuni na hivyo kuathiri afya zao.

“Katika kuunga mkono juhudi za Serikali tuliamua kuwasiliana na Oryx na tunashukuru wameitikia mwito uliopelekekwa na Mbunge wetu na Waziri wa Fedha Dk.Mwigulu Nchemba…

“Tumeungana kuhakikisha wananchi wa Iramba wanaingia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo inafaida nyingi ikiwemo kuokoa muda wa kupika chakula maana sio lazima kuandaa moto.


“Kupika kwa gesi kunaokoa muda kwa watoto wanaoshindwa kwenda shule wakati mwingine kwa ajili yaa kwenda kuokota kuni na kuandaa mkaa.Pia tunaokoa mazingira yetu kwa sababu ya kukata miti kwa ajili ya kuni na kuandaa mkaa.Kwahiyo matumizi ya gesi yanakwenda kuondoa tatizo hilo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!