Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM wampa maagizo mazito Waziri Makamba
Habari Mchanganyiko

CCM wampa maagizo mazito Waziri Makamba

Spread the love

 

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amemuagiza Waziri wa Nishati, Januari Makamba kuhakikisha umeme wa REA unawaka mwezi Aprili katika vijiji vyote vya mkoani Morogoro kama alivyoahidi. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).

Chongolo alisema hayo jana akiwa katika Kijiji Cha Dumila Juu kata ya Dumila baada ya kupokea kero ya umeme kwenye maeneo mbalimbali ya mkoani hapa ikiwemo eneo hilo akiwa kwenye ziara yake ya siku tatu mkoani hapa kukagua miradi na shughuli za maendeleo pamoja na kuangalia uhai wa Chama.

Alisema pia alipokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa kijiji hicho juu ya ukosefu wa umeme katika vijiji 60 vilivyopo chini ya mradi wa maji kupitia mradi wa usambazaji nishati vijijini (REA) awamu III mzunguko wa pili.

Chongolo alisema Rais Samia Suluhu Hassan alitenga na kupeleka fedha mkoani Morogoro kwa ajili ya kupatikana umeme katika vijiji mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi ambapo alipomuuliza Waziri Makamba aliahidi kuwasha umeme katika vijiji vya Morogoro mwezi Aprili mwaka huu.

Akizungumzia kuhusu umeme meneja wa TANESCO Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Fadhili Chilombe alikiri vijiji 55 kati ya 60 kutowekwa umeme kwa wakati unaohitajika kufuatia mkandarasi mwenye kampuni ya HNXJDL INT CONTRUCTIRS kutokuwa na utekekezaji mzuri wa mradi huo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo

Hivyo Mhandisi alisema TANESCO itahakikisha kazi hiyo inakamilika na vijiji vyote vinavyohusika kupata umeme kwa wakati licha ya mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha usambazaji huo tangu Agosti mwaka 2021 aliposaini mkataba hadi kuonekana kushindwa kukamilisha itakapofika mwisho wa mkataba wake Februali 28 mwaka huu.

Hata hivyo meneja huyo aliwahakikishia wananchi wa vijiji 60 vya kata ya Dumila kuwapunguzia bei ya gharama za huduma za umeme kutoka 321,000 iliyopo kwa Sasa hadi kufikia 27,000 inayopaswa kulipia kupitia REA.

Mhandisi Chilombe aliwaasa wananchi wa vijiji hivyo kuwa tayari kibadilishiwa gharama ya huduma hiyo pale kata hiyo itakapopewa hadhi ya kuwa mji mdogo sababu kuwa mji mdogo ni sehemu ya kuonekana kukua katika kila nyanja ikiwemo kiuchumi.

“Wapo watu wanakaa kwenye miji lakini hawana hadhi hiyo na wanaendelea kulipa gharama kubwa za kuingiza umeme, mkishapata hadhi ya kuwa mji mdogo nitarudi tena kuangalia vijiji vyenye hadhi na kuwarudisha kwenye huduma kubwa ya kuingiziwa umeme” alisema Mhandisi Chilombe.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba

Awali Mwenyekiti wa shina namba 10 balozi, Bakari Kimario alimuomba katibu mkuu huyo kuipa hadhi ya mji mdogo kata ya Dumila kutokana na kuendelea kukua kwa kasi kila kukicha.

Pia alimuomba katibu huyo kuwasaidia ili wapunguziwe gharama kubwa za kuingiza umeme kwa sababu ni changamoto kubwa kwao katika kupiga hatua za maendeleo.

Katika mkutano huo wa hadhara Mwenyekiti wa Jimbo la Mikumi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bakari Kilo Hassan alirejea CCM akidai kuridhishwa na itendaji kati wa Rais Samia ambaye anaonesha njia ya maendeleo kiuchumi na kisiasa kwa vyama vyote ambapo haoni sababu ya kuendele kuwa CHADEMA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!