Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo: Chama hakitaacha kuhoji, kufuatilia miradi
Habari za Siasa

Chongolo: Chama hakitaacha kuhoji, kufuatilia miradi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo
Spread the love

 

KATIBU mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema Chama hicho hakiko tayari kuacha kuhoji na kufuatilia kwa Ukaribu Miradi mbalimbali ya Kimaendeleo na Kimkakati inayotekelezwa na Serikali. Anaripoti Christina Haule, Kilosa …(endelea).

Chongolo ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Januari, 2023 katika Kata ya Dumila, Wilaya ya Kilosa aliposhiriki kikao cha shina namba 10, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani Morogoro, ambapo pia alipata nafasi ya kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi kwenye kata hiyo.

Amesema CCM ndio chama kinachoongoza serikali ya sasa iliyopo madarakani, hivyo ni jukumu lake kuendelea kuhoji na kufuatilia kwa sababu ndio kimepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania.

“Kuna jamaa wajanja wanataka tusihoji wala kufuatilia, sisi lazima tufuatilie, tuhoji na tuambiane ukweli hadi kieleweke kwa sababu CCM ndio iliyopewa dhamana na wananchi ya kuongoza nchi,” amesema Chongolo.

Aidha Chongolo amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), hakiko tayari kuharibikiwa ndio maana kinapita kwa wananchi na kila eneo ili kutimiza wajibu wake kwa Watanzania ili kuona kama ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 inatekelezwa kikamilifu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema

Kwa upande wake Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, amewataka viongozi na watendaji mbalimbali waliopewa dhamana kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kwenye maeneo yao.

” Kazi yetu kubwa sisi wanachama wa Chama cha Mapinduzi ni kuendelea kuisimamia Serikali ili iweze kutatua hizo kero ikiwemo kuizungumzia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ili wananchi waweze kutambua umuhimu wake kwa ajili ya maendeleo ya Taifa” amesisitiza Mjema.

Aidha katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mikumi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Bakari Hasani amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema ameridhika na kazi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sijalazimishwa na mtu yoyote sijagombana na ndugu zangu wa Chadema,najua matusi yatakuwa mengi ila hakuna tusi jipya.Nimeona sura aliyoonesha mama Samia kwenye ujenzi wa taifa, acha nije kumuunga mkono,” amesema Hasani.

Tukio hilo limefanywa leo katika Kijiji cha Dumila Juu wilayani Kilosa mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Morogoro ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama ngazi ya mashina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!