Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashe apewa siku saba kuhakikisha skimu za umwagiliaji zinafanya kazi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Bashe apewa siku saba kuhakikisha skimu za umwagiliaji zinafanya kazi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo
Spread the love
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amempa siku 7 Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kufika katika Kijiji Cha Mvumi Wilayani Kilosa mkoani hapa kuhakikisha skimu ya umwagiliaji iliyopo na za mkoa mzima zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa. Anaripoti Christina Haule, Kilosa … (endelea).Chongolo alisema hayo jana akiwa kwenye Kijiji Cha Mvumi kata ya Mvumi Wilayani Kilosa wakati akiwa kwenye ziara ya siku 9 mkoani hapa ambapo alisema katika Kijiji hicho Kuna skimu ya umwagiliaji ambayo haifanyi kazi huku kukiwa na uongozi usio sahihi.

Hivyo alimuagiza Waziri huyo wa Kilimo kuhakikisha anaweka mameneja kwenye kila skimu za umwagiliaji mkoa ili waweze kutoa huduma za karibu na kuepusha migogoro ikiwemo ya mipaka kwa wakulima na wafugaji.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Mercy Maneno alisema licha ya kuwa na ardhi nzuri na ya rutuba lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mazao kulingana na kilimo kutokana na kukosa mabwawa makubwa ua kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo Cha umwagiliaji.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema

Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema aliwataka wananchi, wanachama na wapenzi wa CCM kuendelea kutangaza sera na Ilani ya CCM kwa kutangaza mazuri yote aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema kwa Sasa Tanzania Kuna shule Nzuri ambazo wanafunzi wengi hupata elimu bure kuanzia darasa la sifuri Hadi kidato Cha sita Mambo ambayo alisema kuwa yote ni mipango na utekekezaji Ilani ya Chama.

Hivyo aliishauri jamii na wanachama wa CCM na wasio wa CCM kukaa tayari kusubiri mafunzo ya sera na itukadi ya CCM yatakayotokewa hivi karibuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!