Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kijana ahukumiwa jela maisha kwa kubaka mwanafunzi
Habari Mchanganyiko

Kijana ahukumiwa jela maisha kwa kubaka mwanafunzi

Mahakama
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Shinyanga imemuhukumu kifungo cha maisha jela Hamza Butondo (32) baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa miaka 13.

Pia inadaiwa alimtishia kumchoma kisu mwanafunzi huyo iwapo angetoboa siri kwa unyama aliomtendea. Anaripoti Paul Kayanda …(endelea).

Akisoma hukumu hiyo mbele ya Mahakama hiyo, Hakimu mkazi Yusuph Zahoro alidai kuwa mahakama imemhukumu adhabu hiyo mtuhumiwa huyo baada kulidhibitika pasi na shaka kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alidai kuwa mahakama kwa kuzingatia sheria na ushahidi uliotolewa, mazingira ya utendaji wa kosa lenyewe amejiridhisha pasipo na shaka kwamba mshtakiwa anastahili adhabu hiyo.

Hakimu huyo alidai kuwa mshtakiwa huyo tarehe 11 Disemba 2022 maeneo ya Mhunze wilayani Kishapu mkoa wa Shinyanga muda wa saa 10 usiku.

Amedai alitenda kosa hilo kwa binti wa miaka 13 na kumtoa ndani na kumpeleka nje ya nyumba kwenye mto na kumfanyia unyama huo huku akimtishia kumchoma kisu iwapo atatoa siri.

Hata hivyo, Wakili wa Jamhuri, Jukaeli Jairo aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa kwa mshtakiwa huyo sababu mazingira ya kosa.

Pia wakili huyo alidai kuwa mshitakiwa katika maeneo anayoishi ni tishio katika jamii na pia ni mshtakiwa mwenye matendo ya kutisha na anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo yako mahakamani hayajatolewa uamuzi.

Katika utetezi wake mshtakiwa Hamza Butondo aliiomba mahakama isimpe adhabu kali kwani anao watoto pia wazazi wake wanamtegemea na kwamba hawana wa kuwasaidia

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!