Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CBE kuanza kutoa mafunzo ya akili bandia
Elimu

CBE kuanza kutoa mafunzo ya akili bandia

Spread the love
CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeingia makubaliano na Taasisi ya Teknolojia ya Habari JR Institute of Information and Technology ambao utakiwezesha chuo hicho kutoa mafunzo ya akili bandia na usalama wa mitandao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Makubaliano hayo yalisainiwa jana kwenye chuo cha CBE baina ya Mku wa chuo hicho, Profesa Tandi Lwoga na Meneja wa JR Institute, Isack Marandu.

Akizungumza kwenye tukio hilo, Profesa Lwoga alisema ushirikiano huo utakuwa na manufaa makubwa kwa chuo hicho kwani taasisi ya teknolojia ya JR ambayo inafadhiliwa na taasisi ya Punjani Charitable Trust, imebobea kwa kiwango kikubwa kwenye eneo la teknolojia.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga kulia akisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Meneja wa taasisi ya JR Institute of Information Technology, Isack Marandu jana kwenye ofisi za CBE Dar es Salaam.

“Wamechukua walimu wetu 12 kwenye Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ambao watawapa mafunzo yatajayotusaidia nasisi kuanza kufundisha masomo hayo kwenye mwaka wa masomo kuanzia mwakani,” alisema Profesa Tandi

Alisema walimu wa chuo hicho wanasoma masomo hayo kwa njia ya mtandao na wamekuwa wakisoma kozi tofauti tofauti ikiwemo ya akili bandia ambayo imekuwa hitaji kubwa kwenye sehemu mbali mbali duniani.

“Walimun wetu wanafanya Stashahada ya Juu ya intelijensia ya jamii, watatu wamekwenda kusoma stashahada ya juu ya usalama mitandao, wawili wanasoma Stashahada ya Juu ya uchambuzi wa taarifa na sayansi na mmoja anafanya Stashahada ya Juu ya intelijensia ya bishara,” alisema

Aidha, alisema walimu hao wa CBE watasoma kwa njia ya mtandao kwa muda wa miezi 12 na wakimaliza watakuja kuanzisha program hizo walizosomea kwajili ya kuanza kuwafundisha wanafunzi hao.

Alisema baada ya mafunzo hayo anatarajia CBE itaanza kutoa mafunzo yanayoendana sana na sayansi na teknolojia kwani dunia ya sasa inaendeshwa na teknolojia mbalimbali za kisasa ikiwemo ile ya akili bandia.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Tandi Lwoga kulia abadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Meneja wa taasisi ya JR Institute of Information Technology, Isack Marandu jana kwenye ofisi za CBE Dar es Salaam.

“Tunashukuru sana kwaajili ya huu ushirikiano ambao utajengea walimu wetu uwezo kwaajili ya kuanza kutoa mafunzo mafupi mafupi, kufanya tafiti mbalimbali na kutoa ushauri wa kitaalamu nasisi wakimaliza tutaanza kutoa mafunzo kama hayo hayo,” alisema Profesa Lwoga

Mkuu wa Idara ya Hesabu na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), wa CBE, Dk. Ahmed Kijazi, aliushukuru uongozi wa chuo kwa juhudi za kuona umuhimu wa idara hiyo kwenda mbele katika teknolojia hiyo ya kisasa kama akili bandia  na usalama mitandaoni.

Alisema wataalamu wa fani hizo ni wachache na kwamba anaminani uhusiano wa CBE na JR kutaboresha ufundishaji na kupata wahitimu wengi wa fani hiyo maeneo mengi nchini.

“Si kwamba hawa walimu wakihitimu watakuwa na manufaa hapa CBE tu, watakuwa na msaada nchini kwa ujumla kwasababu wataalamu ni wachache sana kwa hiyo watafundisha watu wengi na hatimaye tutapata wataalamu wengi wenye ujuzi wa aina hii,” alisema

Naye Meneja wa JR Institute, Isack Marandu alisema walimu wa CBE wanaendelea kupata mafunzo kwenye chuo hicho na kwamba wanatengeneza walimu ambao watakuwa msaada kwenye teknolojia ya kisasa kama ya akili bandia na usalama mitandao.

Alisema taasisi yao ina wataalamu wa kutosha waliobobea kwenye mafunzo ya akili bandia na usalama wa mitandaoni ambao wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa njia ya mtandao.

Chuo cha CBE kina matawi katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!