Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri
Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the love

RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2022/2023 imbeinisha kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ilitoa hati za ugawaji wa maeneo ya uwindaji (vyeti namba TAWA.0003, TAWA.0004 na TAWA.0005) kupitia makubaliano ya Eneo Maalumu la Uwekezaji kwa Wanyamapori kwa wawekezaji wawili kwenye jumla ya maeneo 13, ingawa maeneo hayo hayakupata idhini ya waziri kuwa vitalu vya uwindaji kama inavyotakiwa kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma jana Jumatatu na CAG Charles Kichere imesema hali hiyo inaonesha kuwa, menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania haikuzingatia majukumu ya Waziri wa Maliasili na Utalii kabla ya kutoa hati husika.

“Ni maoni yangu kuwa, kutoa hati hizo kwa maeneo ambayo hayajapata idhini ya waziri ni kukiuka kwa kiasi kikubwa Kanuni za Eneo Maalumu la Makubaliano ya Uwekezaji wa Wanyamapori za Mwaka 2020 na kuleta shaka kuhusu uwazi na uadilifu wa mchakato wa ugawaji wa maeneo hayo.

“Napendekeza Serikali ihakikishe TAWA inazuia ugawaji wa maeneo maalumu ya uwekezaji kwa wanyamapori bila idhini ya Waziri,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!