Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia
Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the love

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye ametoa wito kwa wafanyabiashara, wanasiasa na wanahabari wamtetee Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, dhidi ya kashfa zinazotolewa mitandaoni dhidi yake.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Nape ametoa wito huo jana Jumatatu baada ya kuibuka matusi na kashfa mitandaoni dhidi ya Rais Samia, kwa madai kuwa ameshindwa kuiendesha nchi.

Waziri huyo wa habari, amevitaka vyombo vya habari kueleza mazuri yaliyofanywa na Rais Samia katika sekta hiyo, ikiwemo kuvirejeshea uhuru vile vilivyofungwa.

“Wanahabari wenzangu ambao vyombo vya vilifungiwa walikuwa wanafanya kazi kwa hofu, mitandao iliyofungiwa twendeni tukaiambie dunia tunasimama na Rais Samia, tunataka tuwaambie fitina zao, chuki zao, sisi tumemuelewa mama,” alisema Nape.

Pia, Nape aliwataka wafanyabiashara na wanasiasa kwenda mitandaoni kueleza mazuri ya Rais Samia, ili kuwaziba midogo wanaomsema vibaya kwamba hajafanya kitu.

“Tunaye Rais mmoja, tusimame tumtetee. Tusimame naye na bila shaka tutaendelea kutoa matunda ya kazi njema alizofanya. Wanasiasa walifungiwa shughuli zao kwa miaka yote, ambao wanafurahia demokrasia iliyoletwa na Serikali ya Samia twendeni tukasimame kila mmoja mtandaoni tukaiambie dunia tunasimama na mama,” alisema Nape na kuongeza:

“Miaka michache iliyopita tulikuwa na wafanyabiashara zinafungwa akaunti zao wanateseka na tax force ya hapa na pale kwenye ukusanyaji wa kodi leo mambo yao yanakwenda sawa sawa, mfanyabiashara ambaye umeguswa katika hjilo nenda mtandaoni kaandike jambo ambalo Rais Samia amekugusa nalo.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!