Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bwege: Msiichague CCM hali mbaya
Habari za Siasa

Bwege: Msiichague CCM hali mbaya

Spread the love

SULEMAN Bungara Maarufu Bwege, Mgombea Ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo kwenye jimbo la Kilwa Kusini, amewataka wananchi wa jimbo la Kinondoni kutokukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kwa kuwa chama hicho hakijaimarisha uchumi wa wananchi. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Bwege ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020,  kwenye uzinduzi wa mkutano wa uzinduzi wa  kampeni ya Saed Kubenea Mgombea Ubunge wa Kinondoni kupitia ACT-Wazalendo.

Bwege huku akiwauliza wananchi kuwa hali ya uchumi kati ya utawala wa awamu ya nne na tano hali ilikuwa ngumu wananchi walijibu awamu ya tano.

Serikali ya awamu ya nne iliongozwa na Rais Mstaafu Jakaya  Mrisho Kikwete na ya tano imeongozwa na Rais John Magufuli ambaye anagombea urais kutimiza muhala wa pili katika awamu yake.

Bwege amesema, ugumu wa kimaisha umesababishwa na utawala wa CCM kwa kuwa imeshinda kusimamia Sera zake.

“Serikali ya CCM ilisema kuwa itakuwa na utawala bora lakini wamekwenda kinyume kwa kuwa haiwezi kuzisimamia sera zake,” amesema Bwege

Watu wa CCM, ACT-Wazalendo, Chadema wanasema hali mbaya na kwamba wakati wa Kikwete hali ilikuwa afadhali.

Amesema wananchi wa Kinondoni hawastahili kumpigia  kura Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CC ) kwa kuwa kipindi chote walishusha wananchi kiuchumi kwa kuwachomea moto nyavu  za wavuvi, walishusha bei mazao ya biashara ya korosho, mbaazi na Ufuta.

Wakati huo huo, amewataka wananchi wa Kinondoni kutomchagua Abbas Tarimba wa CCM kwa kuwa anajihusisha na shughuli haramu kiimani ya kuchezesha mchezo wa bahati nasibu.

Amesema Kinondoni itakasirikiwa na Mwenyezi Mungu endapo itachagua kuongozwa na kiongozi anayesimama mstari wa mbele kufanya shughuli ambazo Mwenyezi Mungu amezikaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!