TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema watu wanaofurika kwenye mikutano yake ya kampeni za urais, hajui kama ni wapiga kura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza jana Jumamosi tarehe 26 Septemba 2020, Lissu alitoa kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi siri ya mafanikio ya kampeni zake kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi.
Akifafanua swali hilo, Lissu alisema chama chake hakijafanya utafiti kujua kama wanaofurika kwenye mikutano hiyo ni wapiga kura, “chama changu hakijafanya utafiti kujua kama hawa wamejiandikisha kupiga kura.”
Akizungumzia uwekaji wa mabango ya wagombea kama ilivyo kwa chama tawala, Lissu amesema chama hicho kinaendelea na michango yake na kwamba, watafanya hivyo nchi nzima.
Hata hivyo, alisisitiza kwamba, mabango hayo kwa kuwa sio ya biashara kwa maana ya kuzalisha pesa, hawatakubali yang’olewe na yaking’olewa watayarudisha.
Leave a comment