Saturday , 15 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu aingia matatani, aitwa NEC
Habari za Siasa

Lissu aingia matatani, aitwa NEC

Tundu Lissu, mgombea wa Urais wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imemuita Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema katika kikao cha kamati ya kitaifa ya maadili tarehe 29 Septemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea)

NEC imesema, Lissu anapaswa kufika siku hiyo ili kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema kuwa Dk. John Pombe Magufuli, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikutana na wasimamizi wa uchagunzi nzima nchi nzima.

Hayo yamesemwa leo Jumapili tarehe 27 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera alipozungumza na waandishi wa habari jijini Arusha alikokwenda kwa ajili ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020.

Dk. Mahera amesema, wakati kampeni za uchaguzi huo ukiendelea, tume imekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wagombea kutoa maneno ya kashfa dhidi ya wagombea wengine na tume yenyewe kinyume na kanuni za maadili.

Amesema, uchaguzi huu unasimamiwa na sheria za Tanzania na “lazima tufuate utamaduni tuliojiwekea. Tume inawasihi wagombea kutumia fursa hii vizuri ili wanaokwenda kusikiliza sera na si matusi.”

“Kitendo cha baadhi ya wagombea wa urais hasa mgombea wa Chadema, Tundu Lissu kuikashfu tume kuwa itaiba kura zake ni kitendo cha kuidhalilisha na kuitisha tume ili isitekeleze wajibu wake kwa uhuru,” amesema Dk. Mahera

“Hili halikubaliki na kamwe tume haitatishwa, kama unajiona umeshinda kwa nini unafanya kampeni, kaa basi usubiri kutangazwa na wagombea wa aina hii wanapaswa kupuuzwa,” amesema.

 

“Tume inasikitishwa na taarifa za uongo, uzishi na upotoshaji zilizotolewa na Tundu Lissu jana tarehe 26 Septemba 2020 huko Musoma akisema Dk. John Pombe Magufuli, mgombea urais wa CCM alikuwa ameitisha kikao tarehe 25 an 26 Septemba 2020 Dodoma aliitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo nchi nzima kwa lengo la kupanga mikakati ya kuhujumu uchaguzi.”

“Lakini pia, tarehe 25 Septemba 2020 kuna taarifa zilisambazwa mitandaoni zikisema Rais Magufuli amefanya kikao na mkurugenzi wa uchaguizi ambaye ni mimi (Dk. Mahera).”

Dk. Mahera amesema, “taarifa zote hizi mbili ni za uongo, uzushi na zenye kuleta taharuki miongoni mwa Watanzania na kujenga picha kwamba uchaguzi huu hautakuwa huru. Nataka kuwahakikishia Tume iko imara, haitatishwa na hatutaki kutishwa tume na tutatumia sharia na kanuni kutangaza aliyeshinda.”

Amesema kutokana na hayo, Lissu atapaswa kufika katika kamati hiyo ili kutoa maelezo na ushahidi wa alichokisema.

1 Comment

  • Ndugu zangu watanzania muwe makini saana, huyo Lissu ni msaliti nia yake ni kuwaweka nyinyi watanzania ndugu zetu katika hali mbovu ya vita vya nyinyi wenyewe kwa wenyewe. Musikubali kujaribiwa na akemewe saana pamoja na zamira zake mbaya kwa taifa lenyu la amani miaka na miaka.
    Mungu ibariki Tanzania na watanzania woote waishi kwa amani kama kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Mataifa Afrika Mashariki yawasilisha bajeti 2024/2025 inayolenga kukuza uchumi

Spread the loveMataifa manne ya Afrika Mashariki jana Alhamisi yamewasilisha bungeni bajeti...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

Habari za SiasaTangulizi

Bilioni 155.4 kugharamia kicheko cha wastaafu 2022-2030

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amesema jumla ya Sh...

error: Content is protected !!