July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge laagiza uchunguzi ‘Super Market’

Spread the love

 

BUNGE la Tanzania, limeiagiza Serikali ifanye uchunguzi katika maduka makubwa ‘Super Market’, ili kuondoa biadhaa za kughushi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo Jumatano, tarehe 16 Juni 2021 na Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu, baada ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, kusema Serikali iko mbioni kutunga sheria ya kulinda haki na maslahi ya watumiaji nchini.

Mwenyekiti huyo wa Bunge, amedai kwamba, hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la bidhaa za kughushi ‘feki’, katika maduka hayo, hali inayoathiri wanunuzi wake.

“Waziri hebu tumeni watu wenu kwenye Ma-Super Market makubwa, muone dettol (dawa ya kuwa wadudu) na sabuni za kuogea zote feki. Watu wanalipa pesa nyingi, wanatumia vitu sio halali na pesa wanazolipa,” amesema Zungu na kuongeza:

Mussa Zungu

“Chunguzeni Super Market zote mkatizame, dettol ya zamani ukiitia maji inakuwa nyeupe, leo ukiitia maji inakuwa nyeusi. Pamoja na sabuni ambazo zimeandikwa majina, makubwa lakini feki.”

Awali, Kigahe alisema Serikali itatunga sheria hiyo, akimjibu Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Oscar Kikoyo, aliyehoji lini Serikali itaunda mamlaka yenye nguvu ya kulinda haki na maslahi ya watumiaji.

“Mihimili muhimu ya uchumi wa soko ni mamlaka za udhibiti, Tume ya Ushindani (FCC) na mamlaka ya kulinda haki na maslahi ya watumiaji (final consumer). Je, ni lini Serikali itaunda mamlaka yenye nguvu ya kulinda haki na maslahi ya watumiaji nchini?” Alisema Kikoyo na kuongeza:

“Je, Serikali ina mpango gani wa kutunga Sheria ya Kuwalinda watumiaji?”

Katika majibu yake kuhusu maswali hayo, Kigahe alisema “ili kumlinda mlaji tunataka tuwe na sheria ya moja kwa moja, itakayohakikisha inasimamia na kumlinda mlaji.”

Waziri Mkuu akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kigahe alisema katika mwaka wa fedha ujao wa 2021/22, itaanzisha rasmi Baraza la Kumtetea na Kumlinda Mlaji (NCAC), ambalo litakuwa na jukumu la kisheria kusiammia haki za mlaji.

“ Serikali imekamilisha uundaji wa NCAC, ambalo litakuwa na jukumu la kisheria kusimamia haki za mlaji. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha taratibu zauanzishwaji wa Baraza hilo,” alisema Kigahe.

error: Content is protected !!