July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga kushuka Dimbani kesho, dhidi ya Ruvu

Spread the love

MARA baada ya kuwa kwenye mapumziko ya wiki mbili kikosi cha Yanga kesho kitashuka dimbani kwenye muendelezo wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Ruvu Shooting. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo namba … utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkaoa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 1 usiku.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo, huku ikifikilia safari ya ubingwa mara baada ya kubakisha mitano, ikiwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 61, alama sita nyuma ya Simba walikuwa kwenye nafasi ya kwanza.

Katika mchezo huo tutashuhudia kurejea kwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Said Ntibanzokiza ambaye ameonekana akifanya mazoezi na kikosi hiko mara baada ya kuwa nje ya Uwanja kwenuye michezo miwili iliyopita.

Kwa upande wa Ruvu Shooting wao wanarejea Uwanjani, huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwenye mchezo uliopita kwa mabao 3-0, mbele ya Simba kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, Mwanza.

Ligi hiyo iilirejea rasmi jana mara baada ya mapumziko ya wiki mbili, toka timu ya Taifa ilipoingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi uliochezwa tarehe 13 Juni 2021, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

error: Content is protected !!