Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Bulembo aanika faida ujenzi Kituo cha afya Kwafungo
Afya

Bulembo aanika faida ujenzi Kituo cha afya Kwafungo

Spread the love

MKUU wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo amesema fedha kutoka katika Mpango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19, zilizotokana na tozo za miamala ya simu zimefanikisha ujenzi wa Kituo cha Afya Kwafungo kilichopo wilayani humo.

Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa mambo makubwa aliyofanya kwa muda mfupi kwenye sekta ya afya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Bulembo ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumzia ujenzi wa kituo hicho cha afya.

Amesema mbali na ujenzi wa kituo hicho pia fedha hizo zimeiwezesha Wilaya ya Muheza kupata nyumba ya mganga Mkuu.

Kituo cha afya kinachojengwa katika kata ya Kwafungo wilayani Muheza mkoani Tanga, kimeelezwa kuwa ni kati ya alama muhimu katika mapinduzi yanayofanywa kwenye sekta ya afya nchini, kikijengwa kupitia fedha za tozo za miamala ya simu.

Kituo cha afya kwa Kwafungo, kimepokelewa kama ukombozi mkubwa, kikitarajiwa kupunguza msongamano katika hospitali ya Wilaya ya Muheza na kupunguza adha ya umbali wa kufuata matibabu.

Joseph Lazaro ambaye ni mkazi wa kata ya Kwafungo ambapo kituo cha Afya kinajengwa, amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya kitakachowapunguzia umbali wa kufuata Huduma za afya.

Diwani wa kata ya Kwafungo, Gabriel Mathayo, naye ameeleza kwamba kituo hicho kitakuwa ukombozi wa wakazi wa tarafa nzima Bwembwela na maeneo ya jirani kwani kipo katikati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!