July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgogoro Urusi-Ukraine: Je, vita ya tatu ya dunia?

Spread the love

KUMEKUWEPO na kurushiana maneno baina ya Urusi na nchi za Magharibi huku kukiwepo matamshi yanayoashiria kutokea vita vya tatu ya dunia sambamba na matumizi ya silaha za nuklia. Anachambua Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais wa Urusi, Vladimir Putin hivi karibuni alinukuliwa akiagiza majeshi yake kuweka tayari silaha za nyuklia bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Wachambuzi wanasema kauli hiyo ya Putin ililenga zaidi kutishia mataifa mengine kuingilia mgogoro huo, na si kwamba alilenga kutumia silaha hizo.

Leo Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, amerudia tena kutaja silaha za nyuklia akimlaumu Rais wa Marekani, Joe Biden kwa kile alichodai alisema “mbadala pekee wa vikwazo ni vita ya tatu ya dunia”

Lavrov katika tamko lake amesema kama mbadala wa vikwazo utakuwa ni vita ya tatu ya dunia basi lazima itakuwa vita ya nuklia.

Amesema mawazo ya vita ya tatu ya dunia yapo tu kwenye vichwa vya wanasisa wa magharibi na si kwa watu wa Urusi.

“Kama kweli vita vya kweli vinapangwa dhidi yetu basi wenye hayo mawazo lazima wafikirie kuhusu hilo (vita ya nuklia) na kwa maoni yangu hiyo mipango ipo,” amesema.

Ukitazama matamshi ya viongozi wa Urusi utaona kwamba vita ya Ukreini bado ni mbichi sana na inakoelekea inakwenda kuwa mbaya zaidi.

Mrusi kwa kiasi fulani amekuwa mkaidi na sugu kwa vikwazo vinavyowekwa na nchi za magharibi na pengine ni kwasababu bado athari kubwa hazijaanza kuonekana.

Hali inaweza kuwa mbaya zaidi na mapigano yakawa makali pale mrusi atakavyoanza kusikia makali ya vikwazo na akachagua njia ya vita kulipa kisasi dhidi ya wale waliomwekea vikwazo.

Hii inatokana na ukweli kuwa Urusi anaonekana kwa sasa si muumini wa majadiliano na ndiyo maana hakuchagua njia ya majadiliano tangu awali katika kutatua mgogoro huo na badala yake aliamua kuchagua njia ya vita.

Ipo dhana nyingine kuwa endapo Urusi itashindwa katika vita hii basi huenda miaka ya Putin madarakani ikahesabika na kwamba naweza kukumbana na mashtaka ya uhalifu wa kivita katika Mhakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC).

Putin anaweza kuanzisha vita ya nyuklia endapo ataona anakwenda kupoteza na anashindwa kupata kile alichokitaka na hatiamaye kuishia ICC.

error: Content is protected !!