Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko WFP, Farm Afrika waunganisha wakulima wa mtama na masoko
Habari Mchanganyiko

WFP, Farm Afrika waunganisha wakulima wa mtama na masoko

Spread the love

 

WAKULIMA wa zao la mtama katika wilaya sita za Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania, wamehakikishiwa soko la uhakika la zao hilo na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Farm Afrika. Anaripoti Selemani Msuya, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa na viongozi wa mashirika hayo wakati wakizungumza na waandishi wa habari aambao wanatembelea Mradi wa Kilimo Himilivu cha Mtama (CSA), unaotekelezwa katika wilaya za Bahi, Kondoa, Chemba, Chamwino, Mpwapwa na Kongwa.

Mkuu wa Ofisi Ndogo ya WFP Dodoma, Neema Sitta amesema mradi huo ambao umelenga kubadilisha maisha ya mkulima umekuwa na mafanikio mengi kutokana na uhakika wa soko uliopo.

Sitta amesema kwa muda mfupi ambao mradi umeanza wamefanikiwa kufikia wakulima zaidi 22,000 ambao kwa msimu wa mwaka jana wameweza kuzalisha tani 28 na kuingiza zaidi ya Sh. bilioni 13.5 ambazo kwa sasa zipo kwenye mzunguko.

“Moja ya lengo letu kuu likikuwa ni kuongeza thamani ya zao la mtama kwa mkulima ambapo hadi sasa tunadiriki kusema tumefanikiwa kwa kiwango kikubwa, kwani kwa sasa soko la zao hilo lipo juu,” amesema.

Sitta amesema wakulima wa zao la mtama wapatao 22,000 wanauza mazao yao nchini Sudani Kusuni, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na wafanyabiashara wengine,” alisema.

Naye Ofisa Mradi wa Farm Afrika, Wilaya ya Chamwino mkoano hapo, Tomothy Gwandu amesema mradi huo umewezesha kuunganisha wakulima zaidi ya 5,431 na masoko ndani na nje ya nchi.

Amesema Farm Afrika wametekeleza mradi wa CSA, kwa ufanisi kutokana na wakulima kuwa na mwamko mzuri baada ya kuhakikishiwa masoko ya kuuza mtama wao.

“Hapa Chamwino mradi wa CSA unatekelezwa katika vijiji 27 ambapo msimu wa mwaka jana wakulima walizalisha zaidi ya tani 300 ambazo zilinunuliwa na TBL kupitia Kampuni ya Apec International,” amesema.

Ofisa huyo amesema pamoja na masoko wanatoa mafunzo kwa wakulima wanaotekeleza mradi, hali ambayo imekuwa ikiongeza idadi ya wakulima kila msimu.

“Tunatekeleza mradi katika vijiji vya Iringa Mvumi, Idifu, Mwenda, Mgunga, Mkwayungu na vingine ambavyo kwa pamoja vimefanya mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na maendeleo kupitia kilimo cha mtama,” amesema.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Nuru Iringa Mvumi, Monica Matonya amesema kikundi chao kiliingia kwenye mradi wa CSA mwaka 2020 ambapo wamefanikiwa kwa asilimia kubwa kutokana na uhakika wa masoko.

Matonya amesema Farm Afrika na WFP wamewafungua macho na sasa wanatambua kilimo ni mkombozi wa maisha yao.

“Soko la mtama ni la uhakika hapa kijijini kwetu, tunawapongeza Farm Afrika na WFP kwa kutufungulia ukurasa mpya wa maisha yetu,” amesema.

Katibu wa kikundi hicho, Rhoda Macheo amesema kikundi hicho chenye wanachama 22, wanawake 13 na wanaume tisa kimekuiwa cha mfano kijijini hapo.

Macheo amesema WFP na Farm Afrika wamewatoa katika kilimo cha kiholela hadi kulima kitaalam, hali ambayo inawawezesha kuongeza mavuno hadi kufikia tani 10,000.

Kwa upande wake Mwanakikundi Japhat Paul amesema uhakika wa soko kupitia mradi wa CSA umemsaidia kuanzisha ufugaji wa nguruwe ambao wanampatia kipato cha uhakika, huku akiongeza eneo la kilimo kila mwaka.

“Mimi kwa sasa nimefanikiwa kununua nguruwe na ninafuga kwa ajili ya biashara lakini mtaji umetoka katika kilimo cha mtama ambacho nimehakikishiwa soko na Farm Afrika na WFP,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!