Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko BRELA watakiwa kufungua mlango wa kuelimisha umma
Habari Mchanganyiko

BRELA watakiwa kufungua mlango wa kuelimisha umma

Godfrey Nyaisa
Spread the love

MUFTI na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali Mbwana ameitaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, (BRELA) kutoa elimu kwa umma ili waielewe na kufaidika na huduma inazozitoa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sheikh Zubeir ametoa rai hiyo jana tarehe 3 Aprili 2024 katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na BRELA kwa wadau wake iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali na kufanyika Jijini Dar es Salaam.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali Mbwana.

Ameeleza kuwa, wapo watu waliofungua kampuni bila kufahamu jinsi ya kusimamia, BRELA iendelee kufungua milango ili watu wengi wapate kuifahamu taasisi na inachokifanya ili kuwasaidia kufanya biashara kwa mujibu wa sheria.

“Taasisi itoe elimu kuhusiana na masuala ya BRELA kwa kuwa wapo wengi huitaja Wakala lakini hawajui inafanya nini, hivyo ni muhimu kuwaelimisha ili watafahamu huduma zinazotolewa, jinsi ya kuzipata na umuhimu wake,”Alisema Sheikh Zubeir

Akieleza umuhimu wa elimu Sheikh Zubeir amefafanua kuwa mtu huweza kuharibikiwa na mambo mengi asipokuwa na elimu huku akitanabaisha kuwa ujinga ni aibu na hakuna anayeukubali na akauridhia.

Katika hatua nyingine Sheikh Zubeir amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa kwa kuandaa iftar kwa mara ya kwanza na kushukuru kwa kumwalika pamoja na wadau wengine kuwa watu wa kwanza kushiriki katika tukio hilo, na kumsihi kuwa zoezi hilo liwe endelevu.

“Awali nilimuuliza Nyaisa hii ni Iftar ya ngapi kufanya, akanieleza kuwa hii ndio mara ya kwanza zoezi kama hili linafanyika, nampogeza sana kwa kuandaa n ani Imani yangu kwamba mtaendelea kufanya vizuri zaidi,” amesema Sheikh Zubeir.

Awali akimkaribisha Mufti katika hafla hiyo, Nyaisa, alimshukuru Mufti na Sheikh Mkuu kwa kukubali kushiriki katika hafla ya Iftar ya kwanza kwa BRELA na kuahidi kuboresha zaidi sambamba na kuwakumbuka watu wenye uhitaji.

BRELA imeandaa iftar hiyo kwa mara ya kwanza kwa lengo la kuwa karibu na wadau ambapo Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dk. Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali Mbwana alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!