Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo NCCR -Mageuzi, wakili kizimbani kwa kugushi nyaraka za mahakama
Habari za Siasa

Vigogo NCCR -Mageuzi, wakili kizimbani kwa kugushi nyaraka za mahakama

Spread the love

VIGOGO wawili waandamizi katika chama cha NCCR- Mageuzi na mwanasheria mmoja, wamepandishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na kusomewa mashtaka 17 ya kughushi na kutoa nyaraka zilizoghushiwa kwenye mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama ya Wilaya. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam… (endeela).

Washtakiwa hao kwenye kesi hiyo namba 8977 ni Behati Aishakiye (Mpita Bakana) – mshtakiwa namba moja, mshtakiwa namba mbili ni Faustine Sungura ambao wote ni wanachama wa chama hicho na Saulo Jackson Kusakalah ambaye ni Mwanasheria.

Mashtaka hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Is-Haq Kupa na Wakili wa Serikali Sada Mohammed. Watuhumiwa hao wote watatu wamekana mashtaka hayo.

Katika mashtaka hayo watatu hao walituhumiwa kughushi nyaraka ikiwemo muhuri wa Mahakama ya Hakimu mkazi wa Ilala, lakini pia kwa nyakati tofauti walighushi saini ya hakimu Aneth Nyenyema wa mahakama ya Ilala.

Hata hivyo, washtakiwa hao waliomba dhamana mbele ya Hakimu Mfawidhi Is-Haq Kupa na kukubaliwa baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini na kuweka bondi yenye thamani ya Sh. tano milioni.

Mpita Bakana, ni Mwenyekiti wa Bodi ya NCCR- Mageuzi, huku Sungura akiwa ni Mkuu wa Idara ya Taasisi za Vyombo vya Dola na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho.

Katika hatua nyingine upande wa Jamhuri ulieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Kupa kuwa tayari upepelezi wa shauri hilo umeshakamilika na hivyo wako tayari kuendelea na kesi.

Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo Hakimu aliahirisha shauri hilo mpaka tarehe 8 Mei 2024 muda wa saa 5:30 katika Mahakama hiyo ya Wilaya ya Kinondoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!