September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

BOJI: mbwa mwenye maringo, hutumia usafiri wa umma kwenda matembezini

Spread the love

MBWA mmoja aliyepatiwa jina Boji, anapenda kutumia mabasi ya umma, treni na boti kusafiri katika jijini la Istanbul, Uturuki.

Licha ya kwamba hakuna anayejua namna mnyama huyo alivyojifunza kusafiri kwa kutumia usafiri wa umma, mmoja wa madereva wa mabasi ya umeme mjini humo alisema wanamfahamu Boji kama mnyama mwenye adabu.

Anasema tabia yake wakati wa kuingia na kutoka kwenye gari lake inapaswa kuwa mfano kwa abiria wote ambao ni binadamu.

Boji amekuwa akivutia kwa wafuasi wa mitandao ya kijamii na wakazi wengi jiji la Istanbul na kuwashangaza wengi jinsi alivyozoea utamaduni wa safari kama hizo.

 

Aylin Erol, ambaye ni mfanyakazi katika sekta ya usafiri wa reli mjini Istanbul, alisema walishtuka kugundua kuwa Boji hupita kwenye vituo angalau 29 vya treni kila siku.

“Anajua anakokwenda, anajua pa kwenda. Inaonekana anajua anachokifanya,” alisema Aylin Erol.

Safari zake kwa siku zinaweza kufikia umbali wa hadi kilometa 30 kwa siku.

Jambo la kufurahisha zaidi ni kuwa japo ya jiji la Istanbul kuwa na mfumo mgumu sana wa boti, bado ni rahisi kwa Boji kusafiri.

BBC inaripoti kuwa mbwa huyo amewekewa kifaa cha sumaku kilichounganishwa kwenye programu maalumu ya simu ili kusaidia mamlaka kufuatilia hali yake ya afya.

Wafanyakazi wa usafiri huhakikisha kuwa anakula vizuri na kunywa maji vizuri akiwa na uzito wa kilo 42.

Boji sasa ni kipenzi cha wengi mjini humo na amekuwa akipokewa na abiria wengi wanaomsalimia kwa upole na kupiga naye picha.

Umaarufu wa Boji ulimpelekea kuzinduliwa kwa akaunti yake ya Twitter mnamo Septemba 2021, wenye jina @boji_ist na kufikia sasa ana zaidi ya wafuasi 90,000.

error: Content is protected !!