Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Milima, mabonde miaka 15 ya Kampuni ya GF
Habari Mchanganyiko

Milima, mabonde miaka 15 ya Kampuni ya GF

Spread the love

 

WAKATI Watanzania wakisherehekea miaka 60 ya Uhuru tarehe 9 Desemba 2021, siku ambayo Bendera ya mkoloni ilishushwa na kupandishwa ya Tanganyika katika Mlima Kilimanjaro, tarehe kama hiyo mwaka 2007, Kampuni ya uuzaji wa magari na mitambo ya kutengenezea barabara GF Trucks & Equipment’s ilianzishwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kampuni iliyoanzishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa FK motors, Mehboob Karmali ambayo kwa sasa imefikisha miaka 15 huku Karmali akisema haikuwa kazi rahisi kufika walipo sasa kwani jitihada binafsi kwa kushirikiana na wafanyakazi ndio zimewafikisha hapo.

Alisema, mara ya kwanza ilikua ngumu sokoni kutambulisha bidhaa za nchini yaani magari ya FAW ambao wao ndio wauzaji wakubwa wa magari hayo nchini.

Karmali amewashukuru wateja mbalimbali wa taasisi hiyo kipindi hicho Bonite, Asas na Azam ambao kwa miaka hiyo ndio walikua wateja wao wakubwa.

Aidha, mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema kuaminiwa na kuongoza kampuni yenye wafanyakazi zaid ya 200 ni kazi ngumu lakini anashukuru Mungu kutokana na umoja uliopo baina ya wafanyakazi, wateja na uongozi wa kampuni hiyo kazi zinaendelea.

Akikumbuka jinsi walivyoliteka soko la bidhaa hizo za FAW na baadae XCMG nchini ilikuwa hawana namna kuna wakati ilibidi wapiti kwa wateja wakubwa na kuwaomba wachukue magari hayo na mitambo watumie kwa kipindi cha miezi sita kama hayataharibika basi watafaya malipo na ndio mbinu iliwasaidia kufanikiwa lakini ilikua ni kama kujilipua.

Pia, GF ni wauzaji wa Mitambo ya XCMG, WEICHAN, HONY YANG na FAW.

Kwa jitihada hizo siku hadi siku kampuni iliendelea kukuwa na kujitangaza siku hadi siku na leo tunajivunia kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari kilichopo Kibaha mkoani Pwani ni GF- Vehicle Assembly Ltd haya yoote ni matunda ya miaka 15 ya GF

Naye mfanyakazi wa kampuni hiyo, Mhandisi Salum Issa ambae aliibuka mmoja ya wafanyakazi bora alisema kikubwa ni kumshukuru Mungu kwani ukaribu wa viongozi wao kwa wafanyakazi ndio unasababisha wao kujituma na kujitolea pale inapobidi kwa faida ya wafanyakazi na kampuni pia Maswala ya matatizo popote huwa hayakosi muhimu ni kuvumiliana na kuchapa kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the loveDEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya Msingi...

Habari Mchanganyiko

Dereva ajali iliyoua wanafunzi Arusha afikishwa kortini, aomba apelekwe rumande

Spread the love  DEREVA aliyehusika katika ajali la basi la Shule ya...

error: Content is protected !!