May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bobi Wine kuhudhuria kikao cha Baraza kuu la Chadema

Robert Kyagulanyi 'Bobi Wine'

Spread the love

 

KIONGOZI wa Upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine,anatarajia kuwa mgeni maalum katika kiakao cha Baraza Kuu la Chadema litakalofanyika jumatano tarehe 11 mei 2022. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea),

Ujio huo umethibitishwa na Mkurugenzi wa Itifaki,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema leo jumatatu tarehe 9 mei 2022,wakati akizungumza na waandishi kuhusu maandalizi ya kikao hicho, kitakachotanguliwa na kikao cha kamati kuu itakayoketi kesho jumanne mei 10 2022.

Chadema kitafanya kikao cha baraza kuu tarehe 11 Mei 2022, kitakacho kuwa na ajenda tano na kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, watakaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.

Aidha Bobi Wine aligombea urais wa Uganda, kwa tiketi ya chama cha National Unity (NUP), platform katika uchaguzi uliopita.

error: Content is protected !!